Category: Habari

BEKI SIMBA AMCHAMBUA OKWI

NA JESSCA NANGAWE BEKI mpya wa Simba, Jamal Mwambeleko, amechekelea kurejea kwa straika Emmanuel Okwi, kwamba kikosi cha Wekundu hao kitakuwa cha mfano. Mwambeleko aliliambia BINGWA jana kuwa, anaamini ujio wa mshambuliaji huyo utaongeza ushindani katika kikosi chao kinachopambana kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, huku pia kikikabiliwa na michuano ya kimataifa mwakani. “Ni mchezaji mzuri na ataongeza ushindani […]

NYAMLANI AJIENGUA UCHAGUZI TFF

NA ZAITUNI KIBWANA MGOMBEA wa nafasi ya Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Athuman Nyamlani, jana alijiengua katika kinyang’anyiro hicho kutokana na kile kinachodaiwa ni sababu zilizo nje ya uwezo wake. Akizungumza na BINGWA jana, Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas, alisema Nyamlani aliwasilisha barua yake jana iliyoeleza kujitoa kwenye uchaguzi huo. Alfred alisema sababu kuu ya kujitoa kwenye […]

OKWI MAMBO MURUA SIMBA

NA ZAITUNI KIBWANA EMMANUEL Okwi aliyetua nchini juzi usiku ili kumalizana na Wekundu wa MSimbazi, jana usiku pande hizo zilikuwa katika mchakato wa kukamilisha mkataba wa miaka miwili ambao alitarajiwa kuusaini nyota huyo wa Uganda. Okwi alitua juzi na kulakiwa kwa mbwembwe na viongozi wa Simba, akiwamo Makamu wa Rais wa klabu hiyo, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ na kufichwa kwenye moja […]

KIUNGO MBEYA CITY ATEMBEZA SAINI BARABARANI

NA MOHAMED KASSARA KIUNGO wa Mbeya City, Cristian Sembuli, amesema anasaka timu ya kuchezea kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kumaliza mkataba na klabu yake. Akizugumza na BINGWA jana, Sembuli alisema kwa sasa hana mkataba unaomfunga hivyo yuko tayari kuichezea timu yoyote itakayomhitaji. Sembuli alisema wanaendelea kufanya mazoezi binafsi kwa lengo la kujiweka fiti, wakati akisubiri […]

AZAM YASAKA MRITHI WA KAPOMBE NDONDO CUP

NA WINFRIDA MTOI BAADA ya beki wao Shomari Kapombe kusajiliwa na Simba, klabu ya Azam FC  imehamishia majeshi yake katika michuano ya Ndondo Cup inayoendelea jijini Dar es Salaam kusaka mrithi wake. Azam tayari imekamilisha usajili wa wachezaji wanne wapya ambao ni washambuliaji wawili, Mbaraka Yusuf kutoka Kagera Sugar, Wazir Junior (Toto Africans), kiungo Salmin Hoza na kipa Benetict Haule […]

BOSI YANGA AMZUIA KASEKE KUTUA DAR

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, Deus Kaseke, ameshindwa kuondoka mkoani Mbeya kwa safari ya kuja Dar es Salaam kufanya mazungumzo ya kuongezewa mkataba mwingine na klabu yake kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kutokana na kupigiwa simu ya kuliweka kando suala hilo. Kaseke alitakiwa kuwasili jijini Dar es Salaam Ijumaa iliyopita, lakini siku moja kabla ya safari […]

MAJIMAJI WAPIGA HODI KWA MRWANDA

NA SAADA SALIM MAJIMAJI ilikuwa na hali mbaya msimu uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kunusurika kushuka daraja, hali hiyo imewashtua viongozi wa klabu hiyo ambao wameamua kusajili wachezaji wa kazi. Ili kujiepusha na majaribu hayo, uongozi wa Majimaji umepanga kumrejesha kikosini mshambuliaji wao wa zamani, Danny Mrwanda. Taarifa za uhakika ambazo BINGWA limezinasa kutoka ndani ya Majimaji, […]

YANGA NI MAO AU MUDATHIR YAHYA

NA EZEKIEL TENDWA KUONDOKA kwa kiungo wao mahiri Haruna Niyonzima aliyejiunga na Simba, kumewafanya Wanayanga kuelekeza akili zao kwa Himid Mao pamoja na Mudathir Yahya wote kutoka Azam FC, wakielezwa wanaweza kukiimarisha kikosi chao. Japo Mao amekuwa akiikana Yanga, BINGWA lina taarifa za kutosha kwamba mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara wanafanya kila linalowezekana kumchomoa Azam. Kigogo mmoja wa […]