Category: Habari

MWAMUZI WA SIMBA VS MBAO HUYU HAPA

NA ZAINAB IDDY MWAMUZI Ahmed Kikumbo kutoka Dodoma ameteuliwa kuchezesha mchezo wa fainali ya Kombe la FA kati ya Simba na Mbao FC, utakaochezwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Jamhuri, mkoani humo. Akizungumza na BINGWA, Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi, Salum Chama, amesema Ahmed atasaidiana na Mohamed Mkono wa Tanga pamoja na Omary Juma wa Dodoma. Chama alisema uteuzi wa […]

MSUVA, MUSSA WAGAWANA ZAWADI YA MFUNGAJI BORA

NA MWANDISHI WETU WASHAMBULIAJI Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting na Simon Msuva wa Yanga, watagawana zawadi ya ufungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu, baada ya wawili hao kufungana kwa mabao.   Kutokana na wachezaji hao kuibuka vinara kwa kila mmoja kufunga mabao 14, watagawana zawadi ya mfungaji bora ambayo ni Sh 5,800,000.   Yanga imemaliza ligi […]

YANGA YAIPIGA KIJEMBE SIMBA

NA HUSSEIN OMAR WAKATI mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, wakitarajiwa kukabidhiwa zawadi zao za ubingwa kesho na wadhamini Vodacom, Wanajangwani hao wamewapiga kijembe Simba na kuwaambia kuwa, watani wao hao wa jadi ni kama waliwatandikia jamvi kisha wao wakamtwaa ‘mwali’ kiulaini. Jeuri hiyo ya Yanga imekuja siku chache baada ya timu hiyo kufanikiwa kutetea ubingwa wake huo kwa […]

WACHEZAJI MAJIMAJI WAOGA NOTI

NA SHARIFA MMASI BAADA ya kufanikiwa kubaki Ligi Kuu Tanzania Bara, uongozi wa klabu ya Majimaji umelipa madeni yote uliokuwa ukidaiwa na wachezaji wao. Majimaji ilijihakikishia kusalia katika ligi hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa mwisho uliopigwa kwenye Uwanja wa Majimaji, Songea. Katibu Mkuu wa Majimaji, Zacharia Ngaliminayo, alisema jana kuwa […]

AZANIA YAISHIA NUSU FAINALI STANDARD CHARTERED

NA MWANDISHI WETU, WATANZANIA wametakiwa kuziandaa vyema timu zao katika michuano ya Standard Chartered kwa msimu ujao, ili kuhakikisha wanafanya vyema zaidi na kutwaa taji hilo baada ya fainali ya juzi usiku kushuhudia klabu ya Azania ikitolewa kwa penalti 1 – 0, katika hatua ya nusu fainali na wenyeji, Uingereza. Lakini timu hizo zilitoka suluhu pacha katika muda wa kawaida […]

MECKY MEXIME SASA AWA DAKTARI

NA WINFRIDA MTOI BAADA ya kufanikiwa kumaliza katika nafasi ya tatu ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Mexime, amejifananisha na mtu mwenye taaluma ya udaktari. Akizungumza na BINGWA, Mexime alisema aliikuta Kagera Sugar ikiwa katika hali ngumu na kisha kuirudisha kwenye ramani, kitu kinachomfanya ajione kama daktari ambaye kazi yake kubwa ni kuhakikisha anamtibu mgonjwa. […]

AJIB ATUA AZAM FC

NA SAADA SALIM, WAKATI Simba ikiwa kwenye mvutano na Ibrahim Ajib kuhusu kumwongezea mkataba mpya, matajiri wa Azam wameingilia kati vita hiyo ya kuwania saini ya straika huyo. Azam wameingia kwenye vita ya Ajib baada ya kuachana na straika wake, John Bocco, ambaye tayari ameanza harakati za kutafuta timu nyingine kwa ajili ya msimu ujao. Kitendo cha Simba kuendelea kuwa […]

MECKY MEXIME SASA AWA DAKTARI

NA WINFRIDA MTOI, BAADA ya kufanikiwa kumaliza katika nafasi ya tatu ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Mexime, amejifananisha na mtu mwenye taaluma ya udaktari. Akizungumza na BINGWA, Mexime alisema aliikuta Kagera Sugar ikiwa katika hali ngumu na kisha kuirudisha kwenye ramani, kitu kinachomfanya ajione kama daktari ambaye kazi yake kubwa ni kuhakikisha anamtibu mgonjwa. […]

POINTI TATU SIMBA ZATINGA KAMATI YA NIDHAMU FIFA

NA ZAITUNI KIBWANA KLABU ya Simba imedai barua ya sakata la pointi zao tatu walizopewa na kupokwa baada ya Kagera Sugar kumchezesha mchezaji Mohamed Fakhi, ambaye alidaiwa kuwa na kadi tatu za njano, imekwishapokelewa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) na sasa wanachosubiri ni uamuzi wa kamati ya nidhamu. Simba wamepeleka malalamiko yao Fifa dhidi ya Shirikisho la Soka […]