Category: Habari

Simba SC yapiga hodi Zambia, Chile

NA TIMA SIKILO ILI kunasa wachezaji wenye kiwango cha juu watakaouendeleza moto wao waliouwasha msimu huu katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba imepanga kupiga hodi nchini Zambia, Chile, Ivory Coast, DR Congo ambako wanaamini kupata ‘majembe’ hasa. Msimu huu Simba ilifika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kutokana na kuwa na kikosi kipana chenye wachezaji wengi wazoefu wa michuano […]

Yanga kumfanyia umafia Kagere

NA ZAITUNI KIBWANA KIKOSI cha Yanga kimeendelea na mazoezi yake katika Uwanja wa Chuo cha Polisi, Dar es Salaam, huku kocha mkuu wa timu hiyo, Mwinyi Zahera, akisisitiza ushindi ni lazima kesho watakapowavaa Mbeya City. Yanga ndio wenyeji wa mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaopigwa Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, huku wakiweka mkakati kabambe wa kumtengenezea […]

AUSSEMS ‘BYE BYE’ SIMBA

NA MWAMVITA MTANDA KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, yupo mbioni kuachana na timu hiyo, huku uongozi wa Wekundu wa Msimbazi hao ukiwa umeanza mchakato wa kumsaka mbadala wake. Habari za uhakika zilizolifikia BINGWA wikiendi iliyopita, zinasema kuwa kocha huyo amefikia uamuzi huo kutokana na kutoridhishwa na mshahara anaolipwa. Imedaiwa kuwa kocha huyo raia wa Ubelgiji, analipwa kitita cha Dola […]

Bocco aongeza mwaka Simba

TIMA SIKILO HATIMAYE mshambuliaji wa Simba, John Bocco, ameongeza mkataba wa mwaka mmoja zaidi Simba na hivyo kuzima tetesi za kuhusishwa na klabu yake ya zamani ya Azam iliyokuwa imepanga kumrejesha Chamazi, Dar es Salaam. Habari zilizonaswa na BINGWA jana kutoka kwa mmoja wa vigogo wa Simba, zinasema kuwa Bocco ni miongoni mwa wachezaji ambao klabu hiyo haikuwa tayari kuwapoteza […]

Wachezaji: Yanga ingeshuka daraja

HUSSEIN OMAR ZIKIWA zimebaki siku chache kabla Ligi Kuu Tanzania Bara kufikia tamati, wachezaji wa Yanga wamesema kama si Kocha Mkuu wao, Mwinyi Zahera, timu hiyo ingeshuka daraja msimu huu. Nyota hao walitoa kauli hiyo katika hafla ya futari iliyoandaliwa na viongozi wa timu hiyo iliyofanyika juzi katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau kibao […]

Zahera jeuri aisee

NA HUSSEIN OMAR MAMILIONI yaliyokusanywa na klabu ya Yanga kupitia mpango wao wa mashabiki kuichangia, yameendelea kumpa jeuri kocha mkuu wa timu hiyo, Mwinyi Zahera, ambaye ametangaza msimu ujao kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara mapema tu akiwa na mechi kibao mkononi. Sambamba na hilo, Zahera amedai kuwa kutokana na mapenzi yake aliyonayo kwa Yanga, amekataa kitita cha Dola […]

Barca: Valverde ataendelea kuwa hapa

CATALUNYA, Hispania TAARIFA iliyotolewa na Barcelona kupitia rais wao, Josep Bartomeu, imedai kuwa hawana mpango wa kuachana na kocha wao, Ernesto Valverde. Si tu Valverde atakuwa kocha wa Barca msimu ujao, pia ni kocha wa mipango ya muda mrefu ya klabu hiyo, kwa mujibu wa Rais Bartomeu. Valverde alikuwa akiinoa Athletic Bilbao kabla ya kuitwa Camp Nou msimu wa 2017-18 […]

Mpira Pesa Original yajipanga kutengeneza bonge la ofisi

WINFRIDA MTOI MPIRA Pesa ni miongoni mwa matawi ya mashabiki wa Klabu ya Simba yenye nguvu kubwa hapa nchini kutokana na ukongwe wao ikiwemo kushiriki mambo mbalimbali yanayohusu timu. Tawi hilo limekuwa na nguvu na ushawishi mkubwa kwa Wanasimba kutokana na wanachama wake kuwa na msimamo wa kufanya mambo yao bila kuendeshwa na mtu. Tumeshuhudia mara kwa mara, Mpira Pesa […]

Samatta: Ubingwa muhimu kuliko kiatu cha dhahabu

EZEKIEL TENDWA NAHODHA wa Taifa Stars, Mbwana Samatta anayekipiga na timu ya Genk ambayo juzi usiku ilitwaa ubingwa Ligi Kuu ya Ubelgiji, amesema ushindi huo ni muhimu kuliko kiatu cha dhahabu. Samatta mwenye mabao 23 anawania kiatu cha dhahabu na Hamdi Harbaoui raia wa Tunisia anayeichezea Zulte Waregem, ambaye amemzidi mabao mawili. Hata hivyo, Samatta anaweza akampiku Harbaoui katika mchezo […]

Ajib atoweka mazoezini Yanga

HUSSEIN OMAR JANA kikosi cha Yanga kilipiga tizi la kufa mtu katika Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini, huku kikiwakosa nyota wake wanne wa kikosi cha kwanza,  Mrisho Ngassa, Ibrahimu Ajib, Andrew Vicent ‘Dante’, Juma Makapu na Heritier Makambo. Yanga wanatarajia kuvaana na Mbeya City, Jumatano ijayo katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaopigwa Uwanja wa Uhuru, jijini Dar […]