Category: Habari

Simba kuweka historia ya kufungua tawi Simiyu

Na Mwandishi Wetu, Simiyu Zaidi ya mashabiki 200 wa timu ya Simba Sport Club Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, wamekutana kwa lengo la kuanzisha tawi la Simba Mkoani hapo. Mashabiki hao wamekutana leo Jumamosi Machi 23 ,katika Ukumbi wa Silk ulipo mkoani hapo. Ikumbukwe kuwa Tangu kuanzishwa kwa Mkoa wa Simiyu mwaka 2012 hakujawai kuwa na tawi lolote la timu […]

Wachezaji wakongwe waipa mbinu Taifa Stars ya kuiua Uganda

Elizabeth Joachim, Dar es salaam. Wachezaji wa timu ya Taifa (Taifa Stars) wamehaswa kuwa na upendo, ushirikiano na kutokuwa na ubinafsi ili washinde mechi ya kutafuta tiketi ya kufuzu Afcon dhidi ya timu ya taifa la Uganda (The Craners) itakayopigwa Jumapili Machi 24 Uwanja wa Taifa. Wito huo umetolewa na baadhi ya mchezaji wa zamani wa timu ya taifa akiwemo, […]

Stars Taifa lipo nyuma yenu

ZAITUNI KIBWANA NA WINFRIDA MTOI TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, leo inashuka dimbani kucheza na Uganda ‘The Cranes’, katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2019). Mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na Watanzania wengi wapenda soka, utachezeshwa na mwamuzi Eric Canstane kutoka Gabon kuanzia saa 12:00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, jijini […]

Yanga yaandaliwa tiketi ya CAF kibabe

NA HUSSEIN OMAR YANGA imeandaliwa mapokezi ‘bab kubwa’ itakapowasili jijini Mwanza kucheza mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Alliance FC ya huko, lengo likiwa ni kuhakikisha inashinda na hatimaye kuzidi kuisogelea tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao. Mshindi wa michuano ya ASFC, atashiriki kipute cha Kombe la Shirikisho Afrika, wakati bingwa […]

SIMBA NOMA, YATIKISA TP MAZEMBE

ZITUNI KIBWANA NA HUSSEIN OMAR TP Mazembe ya DR Congo imekiri kuwa kupangwa na Simba katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, inaweza kuwa mwisho wa safari yao katika michuano hiyo iwapo hawatakuwa makini, wakikiri kuwa kikosi cha Wekundu wa Msimbazi hao kinachonolewa na Mbelgiji Patrick Aussems, kinatisha. Timu hizo zimepangwa kukutana katika hatua hiyo baada ya […]

Pogba awashukia wabaya wa Sterling

MANCHESTER, England KIUNGO wa timu ya Manchester United, Paul Pogba, ameibuka na kuwakumbusha waliokuwa wanamsema winga wa Man City, Raheem Sterling, kuwa huu ndio wakati wake wa kupewa heshima anayostahili. Pogba alisema Sterling amekuwa hapewi heshima hiyo, tofauti na ilivyokuwa mwaka jana aliposhukiwa kwa madai ya kuchochea suala la ubaguzi kwa kuingilia suala la kinda, Tosin Adarabioyo na Phil Foden. […]

MTIMUENI BWANA! Sarri sasa ni adui namba moja Chelsea

LONDON, England MATUMAINI ya Chelsea kukata tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao yanapanda na kushuka kutokana na mwenendo wao wa kusuasua, hasa kichapo cha mabao 2-0 walichopewa na Everton wikiendi iliyopita. Tayari mashabiki wao wameonesha kumchoka na hawataki hata kumsikia kocha wao, Maurizio Sarri, huku mamia kati yao wakianza kuuza tiketi zao za msimu kwa lengo la […]

Aiyee apania kuvunja rekodi ya Tambwe

NA ZAINAB IDDY KINARA wa mabao katika Ligi Kuu Tanzania Bara, Salim Aiyee, ameweka wazi kuwa atafurahi kama atachukua tuzo ya ufungaji bora msimu huu akiwa amefunga mabao zaidi ya 21. Kauli ya Aiyee mwenye mabao 16 hivi sasa, imeonyesha wazi anahitaji kuvunja rekodi ya straika wa Yanga, Amisi Tambwe, aliyoiweka msimu wa 2015/16 baada ya kutikisa nyavu mara 21 […]

Samatta kuongoza mauaji kwa Uganda

NA WINFRIDA MTOI NAHODHA wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Leodegar Tenga, amempa ujanja Mbwana Samatta anayeshika kijiti hicho kwa sasa ili aweze kukiongoza vyema kikosi katika mechi dhidi ya Uganda, The Cranes. Taifa Stars na Uganda zinatarajia kuvaana kesho katika mchezo wa mwisho wa Kundi L wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa Afrika […]