Category: Featured

Featured posts

KABWILI KUENDELEA KUPETA LANGONI, CHIRWA, BUSWITA KAMA KAWA

NA SALMA MPELI Yanga wamewaalika mashabiki wao katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa leo katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam dhidi ya Njombe Mji kutokana na kuwa na uhakika mkubwa wa kuibuka na pointi tatu. Mabingwa hao watetezi, wataingia dimbani kuvaana na Njombe Mji wakiwa na hamasa baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika […]

OKWI: PIERRE ATANIFANYA NIPENDWE ZAIDI SIMBA

NA SAADA SALIM STRAIKA wa Simba, Emmanuel Okwi, amesema mbinu anazopata kutoka kwa Kocha Mkuu, Pierre Lechantre, kwa  kushirikiana na msaidizi wake, Masoud Djuma, itamuongezea kasi yake ya ufungaji na kuisaidia timu yake hiyo kutwaa taji la Ubingwa Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na kufanya vizuri michuano ya kimataifa. Okwi anaongoza katika msimamo wa wafungaji bora, akiwa ametikisa nyavu mara […]

MAPINDUZI CUP YAINGIZA WANNE ‘FIRST 11’ YANGA

NA SALMA MPELI SIKU chache baada ya kocha wa Yanga, George Lwandamina, kuwasili nchini akitokea kwao Zambia, aliungana na timu yake kwenye mazoezi ya jana asubuhi na kuwaingiza wachezaji watatu kwenye kikosi cha kwanza kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa kesho dhidi ya Mwadui FC. Lwandamina alikuwa kwao Zambia kwenye msiba wa mwanae Mofya, aliyejinyonga baada […]

AJIB LAWAMANI PENALTI YA CHIRWA

NA SAADA SALIM, ZANZIBAR PENALTI aliyoikosa Obrey Chirwa wa Yanga katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi, Zanzibar dhidi ya URA ya Uganda juzi, imezua jambo ndani ya kikosi cha Wanajangwani hao ambapo imemwingiza matatani nyota wao, Ibrahim Ajib. Chirwa alikosa penalti ya tano wakati wa hatua ya matuta baada ya timu hizo kutoka suluhu ndani […]

SIMBA SC YAMKIMBIA CHIRWA ZENJI

NA MWANDISHI WETU SIMBA imetupwa nje ya michuano ya Kombe la Mapinduzi, baada ya kufungwa bao 1-0 na URA ya Uganda katika mchezo uliopigwa jana jioni kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Wekundu wa Msimbazi hao wamejikuta wakiondoka visiwani humo wakipishana na mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa ambaye alifika huko juzi jioni ili kukiongezea nguvu kikosi chake, hasa iwapo wangelazimika kukutana […]

OKWI AWATOA ‘POVU’ SIMBA

SAADA SALIM NA SALMA JUMA KITENDO cha Emmanuel Okwi kutokuwapo kundini Simba, kimeonekana kuzidi kuwatoa povu viongozi wa klabu hiyo, kila mmoja akihamaki pale anapoulizwa juu ya Mganda huyo. Baada ya BINGWA toleo la jana kuripoti kuwa, inadaiwa Okwi aligoma kurejea nchini akiwa kwao Uganda kwa kuwa anaidai Simba, kulizuka mjadala mzito kwenye vijiwe vya klabu hiyo na hata kwenye […]

KUMBE FEDHA ZA CHIRWA ZILITAFUNWA

NA HUSSEIN OMAR IMEBAINIKA kuwa kuna mchezo mchafu uliofanyika na kusababisha mvutano kati ya straika wa kimataifa wa Zambia, Obrey Chirwa na mabosi wake wa Yanga. Chirwa alikuwa mshambuliaji pacha wa Donald Ngoma katika klabu ya FC Platinum ya Zimbabwe kabla ya wote kutua Yanga kwa vipindi tofauti. Baada ya kusimama kwa Ligi Kuu Tanzania Bara kupisha michuano ya Chalenji, […]

TAMBWE: YANGA NAFAHAMU KILIO CHENU

NA MARTIN MAZUGWA MSHAMBULIAJI wa Yanga raia wa Burundi, Amissi Tambwe, ametamba kuendeleza kasi yake ya upachikaji mabao katika mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Mbao, akifahamu nini mashabiki wa timu hiyo wanataka, yaani mabao tu. Mchezo huo ujao wa Yanga wa Ligi Kuu Bara iliyokuwa imesimama kupisha michuano ya Kombe la Chalenji, utapigwa kwenye Uwanja […]

TSHISHIMBI AMTWANGA MTU NGUMI

NA MWANDISHI WETU   YANGA ama kweli hawataki utani kwa jinsi wachezaji wanavyopambana katika mazoezi kuwania namba katika kikosi cha kwanza, kiasi cha kusababisha wachezaji kushikana mashati pale mmoja wapo anapodhani kufanyiwa ndivyo sivyo. Ni kutokana na hali hiyo, kiungo wa timu hiyo, Papy Kabamba Tshishimbi, alijikuta akimpiga ngumi Seleman Yusuph baada ya kinda huyo kuonekana kumchezea ndivyo sivyo mwenzake […]

GEORGE LWANDAMINA AZUIWA ZAMBIA

NA HUSSEIN OMAR   KOCHA Mkuu wa Yanga, Mzambia George Lwandamina, amezuiwa nchini kwao Zambia baada ya kuugua ghafla, hali itakayomfanya kuchelewa kurejea nchini kuendelea na majukumu yake. Akizungumza na BINGWA jana, Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, alisema Lwandamina ilikuwa arejee nchini Jumatatu, lakini kutokana na maradhi aliyoyapata, amelazimika kuwa chini ya uangalizi wa madaktari kabla ya kuruhusiwa kusafiri. “Kocha […]