Category: Featured

Featured posts

Sababu za Wasafi kuchunia harusi ya Harmonize hizi hapa

NA TIMA SIKILO MENEJA wa lebo ya Wasafi Classic Baby (Wasafi), Said Fella, amevunja ukimya juu ya sababu za wasanii wa kundi hilo kutohudhuria harusi ya mkali wa Bongo Fleva, Rajab Kahali ‘Harmonize’. Harmonize alifunga ndoa na mpenzi wake, Sarah katika hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam na kuzua gumzo kwa kutoonekana kwa wanafamilia ya WCB. Akizungumza na BINGWA […]

TP Mazembe yaibeba Yanga CAF

WINFRIDA MTOI NA SISCA MACHABA (TUDARCo) YANGA wamezidi kupata mteremko kuelekea mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zesco utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, baada ya TP Mazembe ya DR Congo kutia mkono wao. Wakati Zesco wakiingia kimya kimya nchini, tayari Yanga wamemaliza kazi baada ya kukusanya kila kitu kitakachowawezesha kuwapiga mabao mengi […]

Mwanza waanza kuandaa kikosi cha kikapu

NA BENJAMIN MASESE, MWANZA UONGOZI wa Shule ya Sekondari ya Mwanza umeunda vikosi  tofauti vya timu ya mpira wa kikapu  itakayoshiriki michuano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa. Akizungumza jijini hapa jana,  Makamu Mkuu wa shule hiyo,  Shukrani Lugaila,  alisema  uamuzi huo umetokana  na kujengewa uwanja wa kikapu wa kimataifa. Lugaila alisema uwanja huo ulijengwa  na  Kampuni ya mafuta ya Moil […]

TFF yazipiga mkwara klabu za FDL

NA GLORY MLAY SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limesema klabu za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) itakayoshindwa kulipa Sh. 315,000,  ikiwa ni ada na leseni ya wachezaji haitashiriki ligi hiyo, itakayoanza keshokutwa katika viwanja mbalimbali nchini. Akizungumza na BINGWA jana, Ofisa Mashindano wa TFF, Baraka  Kizuguto,  alisema kila klabu inatakiwa kulipa Sh. 300,000 ikiwa ni ada ya ushiriki na Sh. […]

Wapinzani wa Malindi, Al- Masry kutua Zenji leo

NA IBRAHIM MAKAME, ZANZIBAR WAPINZANI wa timu ya Malindi katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika Al- Masry ya Misri, leo  wanatarajiwa kuwasili visiwani hapa, tayari kwa mchezo wa  raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika utakaochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Amaan. Kwa mujibu wa Mjumbe wa Kamati ya Mashindano wa Kimataifa wa Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF),  Ali […]

Kocha Toto Africans: Yanga imetupa uimara

NA DAMIAN MASYENENE, MWANZA LICHA ya kuchapwa na Yanga mabao 3-0 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Nyamagana, Mwanza, Kocha wa Toto Africans, Ibrahim Mulumba, amesema wachezaji wake wamepata uimara wa kupambana. Akizungumza na BINGWA mara baada ya mchezo huo, Mulumba alisema mchezo huo  umesaidia kuwajenga uzoefu wachezaji wake wanaojiandaa na Ligi Daraja la Pili Tanzania Bara […]

Wolper awang’ata sikio warembo

NA BRIGHITER MASAKI MWIGIZAJI na mbunifu wa mavazi Bongo, Jacqueline Wolper, amesema kama kigezo cha kuolewa kingekuwa sura, basi yeye angekuwa tayari ameolewa. Akizungumza na Papaso la Burudani jana, Wolper alisema warembo wengi huwa wanajidanganya kuwa uzuri ni sura lakini wanasahau tabia. “Unakuta msichana mrembo sana lakini haolewi kwasababu hana sifa za kuwa mke wa mtu kwa hiyo wasichana warembo […]

Prezzo kugombea ubunge Kenya

NAIROBI, KENYA RAPA mkali kutoka nchini Kenya, Jackson Makini ‘Prezzo’, ametagazwa kujiunga na Chama cha Wiper Democratic Movement kujiweka tayari kuwania kiti cha ubunge katika jimbo la Kibra jijini Nairobi kwenye uchaguzi mdogo Novemba mwaka huu. Akizungumzia hatua hiyo Ofisa Habari wa chama hicho, Onesmus Kilonzo, alisema: “Ni kweli CMB Prezoo amejiunga na WDM ambacho kinaongozwa na Kalonzo Musyoka (aliyewahi […]

Kifo cha Boss Martha chawaliza mastaa

NA JEREMIA ERNEST WATU mbalimbali maarufu wameonyesha kushutushwa na kusikitishwa na kifo cha aliyekuwa mchekeshaji majukwaani na mtandaoni Martha Michael ‘Boss Martha’, aliyefariki dunia jana alfajiri katika Hospitali ya Kisarawe alipokuwa akipatiwa matibabu ya Malaria. Mastaa kama Jacqueline Wolper, Jay Mond, Idris Sultan, Diana Kimary, Beka Flavour, Nandy, Whozu na wengi wengine wametuma salamu zao za pole kupitia mitandao ya […]

Simorix atamba kupaisha Kiswahili Australia

NA SISCA MACHABA (TUDARco) MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva ambaye anaishi nchini Australia, Simon Masanja ‘Simorix Jenerali (The General), amesema ataendelea kutumia Kiswahili katika nyimbo zake ili kuitangaza lugha hiyo. Simorix, anayefanya vyema na wimbo ‘Tunapiga Bao’, ameliambia Papaso la Burudani kuwa ana kiu ya kuipeperusha bendera ya Tanzania katika eneo analoishi nchini Australia. “Unaweza kuona katika wimbo wangu ‘Tunapiga Bao’ […]