Category: Featured

Featured posts

Mbonde aanza mazoezi mepesi

NA ASHA KIGUNDULA BEKI wa zamani wa Simba, Salum Mbonde, ameanza mazoezi mepesi, baada ya kupona jeraha lililokuwa linamsumbua kuanzia msimu wa 2017/2018 wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Akizungumza na BINGWA jana, Mbonde alisema anafanya mazoezi chini ya uangalizi wa daktari wa tiba za michezo nchini, Gilbert Kigadya. Alisema kwa sasa ana wiki mbili tangu aanze mazoezi mepesi huku akisubiria […]

Ndayiragije awatoa hofu Azam

NA TIMA SIKILO KOCHA wa Azam, Etienne Ndayiragije, amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Triangle Unitedya Zimbabwe utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam. Akizungumza na BINGWA jana, Ndayiragije alisema timu yake itafanya vizuri Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya kimataifa. Ndayiragije alisema wamejipanga kufanya vizuri michuano […]

Wachezaji Yanga kuoga noti

NA MOHAMED KASSARA KATIKA kuhakikisha wanamaliza kazi mapema nyumbani, uongozi wa Yanga umeahidi kuwajaza mamilioni wachezaji wao iwapo wataifunga Zesco United ya Zambia katika mchezo wa leo wa Ligi ya Mabingwa Afrika. Mchezo huo wa raundi ya kwanza, utapigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kabla ya timu hizo kurudiana Septemba 25, mwaka huu, nchini Zambia. Timu itakayopita raundi […]

Dull Sykes : Natamani Recho arudi kwenye nafasi yake.

Na RICHARD DEO Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Bongo Flava Abdul Sykes, maarufu kama Dull Sykes amefunguka kuwa ana tamani kumuona mwanamziki Winfirda Josephat ‘Recho kizunguzung’ katika ramani ya muziki baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu. Dull Sykes amesema hayo katika mahojiano na moja ya kituo cha Tv, wakati akizungumza maswala mazima ya muziki kwa ujumla na […]

Zahera ataja bei ya ‘kipensi’ chake

SISCA MACHABA (TUDARCo) NA WINFRIDA MTOI BAADA ya kukumbana na adhabu kutokana na mavazi yake, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, ameweka bayana bei ya ‘mapigo’ yake hayo ambayo ni Euro 900, zaidi ya sh. milioni 2 za Kitanzania. Hivi karibuni, Kamati ya Bodi ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (TPLB), ilimpiga  Zahera faini ya sh. 500,000, kwa kosa la […]

Yanga yatamba iko kamili kuikabili Zesco

Richard Deo, Dar es Salaam Kikosi cha Timu ya Yanga SC, kimesema kipo kamili kucheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Zesco United ya nchini Zambia utakaopigwa kesho katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Hayo yamesemwa na Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Noeli Mwandila wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo […]

Zahera unataka kuitoa Zesco? Msikie huyu

NA TIMA SIKILO KUELEKEA mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika dhidi ya Zesco United ya Zambia utakaopigwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Yanga wamepewa ushauri wa nini wafanye ili wasonge mbele. Mchezo huo ni wa raundi ya kwanza na kwamba timu itakayopita, itatinga hatua ya makundi ya michuano hiyo, wakati ile itakayotolewa, itaangukiwa Kombe la […]