Category: Featured

Featured posts

Straika avunja mkataba kisa baridi

STOCKHOLM, Sweden STRAIKA, Musa Noah Kamara, ameamua kuvunja mkataba wake na klabu ya Trelleborgs kwa madai ya kushindwa kuvumilia hali ya hewa ya baridi iliyopo nchini Sweden. Uamuzi huo wa Kamara umekuja baada ya mshambuliaji huyo kudumu hapo kwa muda wiki moja tu na klabu hiyo ilithibitisha kuachana na kinda huyo mwenye umri wa miaka 19. Kamara alisaini mkataba wa […]

WANATISHA Liverpool yamkosha Klopp, ataja siri ya ubingwa Ulaya

LONDON, England KOCHA wa timu ya Liverpool, Jurgen Klopp, amedai kwamba aina ya soka walilocheza dhidi ya Southampton si la kisasa, lakini ni mbinu ya upambanaji ambayo imewafanya kutambulika kama mabingwa wa Ulaya. Liverpool iliichapa Southampton mabao 2-1 katika mchezo huo wa Ligi Kuu England uliochezwa wikiendi iliyopita, lakini safu yao ya ulinzi ilionyesha udhaifu mkubwa mbele ya mlinda mlango, […]

Martial: Mfumo wa Solskjaer usipime

MANCHESTER, England MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Anthony Martial, amesema mfumo anaotumia kocha wao, Ole Gunnar Solskjaer, umemfanya kurudisha ubora wake. Hivi karibuni, Martial alirudishiwa jezi yake ya zamani namba 9, ambayo aliwahi kuivaa kipindi anakipiga Monaco mwaka 2015. “Ni jambo zuri kwa upande wetu, hata safu ya ulinzi ipo imara, inatufanya tucheze kwa uhuru. Mfumo mzuri pia umetusaidia kubadilishana nafasi, […]

Kipa RB Leipzig si kwa majigambo hayo

BERLIN, Ujerumani MLINDA mlango wa RB Leipzig, Peter Gulacsi, amewatambia wapinzani akiwataka kujiandaa kwa vipigo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Union Berlin wikiendi iliyopita. Gulasci, amesema hawana hofu hata kama watacheza na wababe wa ligi hiyo, Bayern Munich na Borussia Dortmund. “Timu yetu ni changa kila mtu anafahamu, msimu uliopita tulikuwa na kiwango bora, tunataka […]

Mancini awaonya wachezaji Italia

MILAN, Italia KOCHA wa timu ya taifa ya Italia, Roberto Mancini amewataka wachezaji wa kikosi hicho kuongeza juhudi ili kuwa na kikosi imara zaidi. Kati ya wachezaji hao, yupo Mario Balotelli ambaye amemtaka kutulia na kucheza kwa kiwango cha juu katika klabu yake mpya ya Brescia. “Nina wachezaji wazuri katika kikosi change, wakiwamo Federico Chiesa, Nicolo Zaniolo, Stefano Sensi na […]

Felix aanza na gundu Atletico

MADRID, Hispania NYOTA mpya wa Atletico Madrid, Joao Felix ameumia mguu wakati timu yake ilipokuwa ikimenyana na Getafe juzi ukiwa ni mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu ya Hispania. Felix alilazimika kutoka uwanjani dakika 65 ya mchezo huo, huku nafasi yake ikichukuliwa na Marcos Llorente. Atletico iliibuka na ushindi wa bao 1-0, shujaa wao akiwa ni Alvaro Morata.

Luiz afichua kilichompeleka Arsenal

LONDON, England BEKI mpya wa Arsenal, David Luiz amesema ameondoka Chelsea kwasababu ya kutafuta changamoto mpya katika maisha yake. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Luiz alisema alitaka kubadilisha mazingira mapya baada ya kudumu Chelsea miaka minne. “Mimi ni mtu mwenye tamaa katika maisha, napenda changamoto mpya, inanipa nguvu zaidi ya kuendelea kupambana na hakuna jambo lingine,” alisema Luiz.

Cole atundika daruga

LONDON, England BEKI wa zamani wa Arsenal na Chelsea, Ashley Cole ametangaza kustaafu kucheza soka akiwa na umri wa miaka 38. Cole, aliachwa na Derby County iliyokuwa ikinolewa na Frank Lampard, msimu uliopita. Akizungumza na kituo cha televisheni cha Sky Sports, Cole alisema kwasasa anafikiria kujiweka katika masuala ya ukocha. “Nimeamua kuacha kucheza soka, nimefikiria kwa kina kabla ya kufanya […]

Miss Tanzania 2019 moto ni ‘fire’

NA PENDO HAMISI (TUDARCo) IKIWA ni siku chache kabla ya fainali za Miss Tanzania 2019, washiriki wameendelea kujifua vilivyo kuhakikisha wanatoa shoo ‘bab kubwa’ Ijumaa hii. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni ya The Look, waandaaji wa mashindano hayo, Basila Mwanukuzi, jumla ya warembo 20 wanatarajiwa kupanda jukwaani kuwania taji linaloshikiliwa na Queenelizabeth Makune. Alisema kuwa shindano hilo la aina […]