Category: Burudani

20 Percent ahofia kuzeeka masikini

NA ESTHER GEORGE MSANII wa Bongo Fleva, Abas Kinzasa ‘20 Percent’, amewaasa vijana kuwa na matumizi sahihi ya fedha, kuepuka starehe zisizo na maana kwani ujana una mwisho wake. Akizungumza na Papaso la Burudani, 20 alisema yeye anahofia kuzeeka akiwa masikini, ndiyo maana yupo makini katika matumizi ya fedha kipindi hiki cha ujana ili atakapozeeka asipate tabu. “Haya maisha ni […]

Hamisa Mobetto ainogesha ‘Zero Player’

NA CHRISTOPHER MSEKENA NYOTA wa filamu za Tanzania, Hamisa Mobetto, mwishoni mwa Oktoba anatarajia kuonekana kwenye filamu ya kimataifa inayoitwa Zero Player, iliyowakutanisha mastaa mbalimbali kutoka Bongo na Afrika Kusini. Mwandaaji wa filamu hiyo, Allan Upamba ‘Allan The Great’, ameliambia Papaso la Burudani kuwa lengo la kuwakutanisha mastaa wa Tanzania na Afrika Kusini ni kutaka kupata utofauti utakaochangia mabadiliko kwa […]

TAARIFA KUTOKA UONGOZI WA SIMBA SC KWA VYOMBO VYA HABARI

SIMBA SPORTS CLUB DAR ES SALAAM 29-6-2016 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Klabu ya Simba inayo furaha kubwa ya kutangaza kumshukuru mlezi wake bwana Mohammed Dewji kwa kuanza kutekeleza ahadi zake kwa vitendo. Dewji maarufu kama MO tayari ameshaanza kulipia mishahara ya wachezaji,benchi la ufundi na Sekretarieti ya klabu na atafanya hivyo katika kipindi chote cha mpito kuelekea mabadiliko ya […]

Sia Pius; Miss Sinza 2016 aliyepania kubeba taji la Miss Tanzania

NA BEATRICE KAIZA KUELEKEA shindano la Miss Tanzania 2016 ambalo washiriki wake wanatarajiwa kuingia kambini Ijumaa hii, Miss Sinza 2016 na mshindi wa tatu Miss Kinondoni, Sia Pius, ametamba kwenda kutwaa taji hilo la mlimbwende wa Tanzania kwa mara ya kwanza tangu shindano hilo lirudishwe. Juzi kati Sia alitembelea Ofisi za New Habari (2006) Ltd, wazalishaji wa magazeti ya Bingwa, […]

Ben Pol akiona cha moto kisa Snura

NA ZAITUNI KIBWANA LICHA ya kukana mara kadhaa kutokuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanadada Snura Mushi, msanii Bernad Mnyelange ‘Ben Pol’, amekiona cha moto baada ya mashabiki wake kumvaa na kumtaka msanii huyo kutolewa sifa. Kauli hiyo ya mashabiki imekuja siku chache baada ya video ikiwaonyesha wawili hao wakiwa kwenye mahaba mazito kwenye maonyesho ya Fiesta yanayoendelea mikoani. Kufuatia […]

Davido akiri ‘kufulia’

LAGOS, Nigeria STAA anayefanya vyema kwenye soko la muziki la Nigeria, Davido, wiki hii ametoa kauli ambayo huenda ikawa imewaacha hoi mashabiki wake. Kwa kile alichokisema nyota huyo, ni wazi amekubali kuwa amepotea kimuziki. Mkali huyo amefunguka kuwa hastahili kupata tuzo yoyote kwa sasa. Mbali na kushinda, Davido amedai kuwa hana uhakika kama anapaswa kutajwa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo […]

Barnaba, Sheta, Ben Pol wafunika Fiesta Tanga

NA MWANDISHI WETU, TANGA BAADA ya kuchengua mikoa ya Dodoma na Morogoro, Tamasha la Tigo Fiesta mwishoni mwa wiki lilihamishia burudani yake mkoani Tanga  ambapo kama kawaida wasanii walipanda jukwaani na kuporomosha burudani ya uhakika kwa maelfu ya mashabiki waliojitokeza kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga. Tamasha hilo la kila mwaka ambapo huendeshwa na Kampuni ya PrimeTime Promotion chini ya […]

Mastaa hawa waliuza bangi, ‘unga’ kabla hawajatoka

LOS ANGELES, Marekani NI watu wachache sana wanaoweza kutojiingiza kwenye njia haramu za kupata fedha wanapokuwa hoi kiuchumi. Kwa kulitambua hilo, wapo wanaoamini kuwa umasikini ni chanzo cha maovu yote. Mtu ‘anapopigika’ ni rahisi kushawishika kujitosa katika uhalifu ili kuingiza kitu mfukoni. Makala haya yanakuletea baadhi ya mastaa ambao kutokana na hali ngumu ya kimaisha kabla ‘hawajatusua’ walijitosa katika biashara […]

Mume wa Angelina Jolie kuchunguzwa na polisi kwa kunyanyasa watoto

LOS ANGELES, Marekani MUME wa mwigizaji nyota wa filamu, Angelina Jolie, Brad Pitt, anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi na polisi kwa tuhuma za kunyanyasa watoto. Mtandao wa TMZ, umesema mwigizaji huyo wa Hollywood, Brad atachunguzwa na polisi na Idara ya Huduma ya Watoto ya Los Angeles, kufuatia shutuma za kuwanyanyasa watoto kwa kuwapiga na kuwatukana. Taarifa zinasema kwamba, Brad mwenye umri wa […]

Pambano la Mayweather, McGregor hakijaeleweka

BONDIA Floyd Mayweather, ameachana na mpango wake wa kuhangaikia pambano lake na Conor McGregor. ‘Money’ ambaye Septemba 2015 alimdunda kwa pointi Andre Berto, alitajwa kuingia ulingoni kuzichapa na mshkaji huyo mwaka huu. Kwa upande wake, Mayweather amedai kuwa McGregor ni mwanamasumbwi pekee ambaye hajawahi kurudiana naye. “Nilijaribu kufanya pambano liwezekane kati yangu na Conor McGregor,” alisema  Mayweather alipokuwa akihojiwa na […]