Category: Burudani

WIZKID ‘PANYA ROAD’ ALIYEOKOLEWA NA KIPAJI CHAKE

LAGOS, Nigeria MAISHA ni vita bwana. Ili uweze kushinda, lazima upambane kweli. Wapo wanaoamini kuwa ‘kutusua’ kimaisha lazima uwe umesoma lakini huenda hiyo si siri pekee. Ni kweli elimu inaweza kurahisisha lakini haimaanishi kuikosa ndio chanzo cha kufeli maisha. Kutambua kipaji ulichonacho na kukipigania ni njia nyingine rahisi ya kufanikiwa. Maisha ya mwanamuziki, Ayo Balogun ‘Wizkid’ yamethibitisha kuwa kipaji kinaweza […]

DIAMOND PLATINUMZ MAJARIBUNI KWA MMAREKANI FUTURE

NA MWANDISHI WETU, MKALI wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’, Julai 22, mwaka huu atakuwa na mtihani mgumu kuthibitisha ubora wake, pale atakapochuana na rappa wa Marekani anayekuja kwa kasi katika muziki kwa sasa, Nayvadius DeMun Wilburn, maarufu kwa jina la Future katika tamasha litakalofanyika viwanja vya Leaders Club, Dar es Salaam. Tamasha hilo litakuwa ni hitimisho la kampeni ya […]

CHRIS BROWN AZINGUA TENA, AMDUNDA MWANDISHI

LOS ANGELES, Marekani HIVI karibuni kumekuwa na madai kuwa afya ya akili ya mwanamuziki Chris Brown si nzuri. Ni kama mshikaji huyo hayuko sawa kiakili. Mara kadhaa amekuwa akihusika katika matukio ya ajabu, huku hali hiyo ikihusishwa na utumizi wa dawa za kulevya. Miezi michache iliyopita, marafiki zake walidai kuwa jamaa haeleweki na amekuwa akiwatimua kazi wafanyakazi wake. Lakini sasa, […]

YOUNG HASSAN ALLY MWIMBAJI, MTUNZI MWENYE NDOTO ZA KUIFUFUA TAARAB

NA SHARIFA MMASI, UNAPOUZUNGUMZIA muziki wa taarab nchini si rahisi kuacha kulitaja jina la msanii Hassan Ally maarufu ‘Young Hassan Ally’. Staili yake ya uimbaji na mashairi yenye vina ndio silaha inayomweka kwenye ramani ndani ya soko la muziki huo hadi sasa. Mkali huyo aliyewahi kutamba na wimbo ‘Chozi la Mnyonge’, hivi sasa yupo katika kundi la Ogopa Kopa Classic […]

AMIN: MUZIKI WANGU SI KAMA ’BIG G’

NA BEATRICE KAIZA, KAMA kawaida Jiachie na Staa Wako lilimtafuta mwanamuziki aliyewika miaka ya nyuma kwenye Bongo Fleva, Amin Mwinyimkuu, maarufu kama Amin na kufanya naye mazungumzo ya hapa na pale kuhusu maisha yake. Hata hivyo, kwa muda mrefu Amin amekuwa kimya, kiasi kwamba mashabiki wake wamekuwa wakihoji yuko wapi msanii huyu ambaye pia ana kipaji cha kutunga. Miongoni mwa […]

KWANINI 50 CENT NA MTOTO WAKE NI CHUI NA PAKA? (2)

LOS ANGELES, Marekani BADO tunaendelea na simulizi ya mgogoro mkubwa uliopo kati ya mwanamuziki 50 Cent na mtoto wake wa kiume, Marquez. Kama ulipitwa na sehemu ya kwanza ya mkasa huo, tambua kuwa hivi sasa wawili hao ni maadui wakubwa na mara kadhaa wamekuwa wakitupiana maneno kupitia mitandao ya kijamii. Kuthibitisha chuki zake kwa mzazi wake huyo, Marquez aliachia ngoma […]

NEY WA MITEGO AMALIZA SHOO KIBABE

NA FESTO POLEA, ZANZIBAR RAPA Emmanuel Elibariki (Ney wa Mitego) amefunga shoo ya kuhitimisha mwisho wa Tamasha la Zanzibar Swahili awamu ya kwanza kwa kufanya shoo ya kibabe iliyopokelewa kwa shangwe kubwa na mashabiki wake waliohudhuria tamasha hilo Ukumbi wa Ngome Kongwe, Zanzibar. Ney aliingia ukumbini hapo akiwa amezungukwa na mabaunsa zaidi ya saba pamoja na idadi kubwa ya wapambe […]

SIASA ITAIRUDISHA BONGO FLEVA ILIKOTOKA

SOKO la muziki wa Bongo Fleva hapa nchini ni moja kati ya vyanzo vikubwa vya ajira kwa vijana. Hakika Serikali isingeweza kulimudu kundi kubwa lililoacha kukaa vijiweni na kuamua kujitosa katika muziki huo. Katika miaka ya hivi karibuni, Bongo Fleva imeweza kuiacha mbali Bongo Movie, ambayo wasanii wake wamejikita zaidi katika kutupiana madongo kupitia mitandao ya kijamii. Kwa kipindi cha […]

AMBER ROSE NAYE HAISHIWI VITUKO

NEW YORK, Marekani AMBER Rose alikuwa amewashtua mashabiki wake na kuanza kujiuliza kama alikuwa amekusudia kutangaza rangi ya mdomo au alilenga kuanika chuchu zake kwa makusudi. Katika picha aliyoweka kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram, alionekana mwanamitindo huyo akilamba rangi yake ya mdomo, huku maziwa yake yakiwa nje na kufanya mashabiki wake kuachana na rangi iliyodaiwa kwamba alikuwa anaitangaza […]

KESI YA WEMA KUPIGWA CHINI

NA MWANDISHI WETU, HAKIMU MkaziMkuu, Thomas Simba,ametishia kuifuta kesi ya kukutwa na kete moja ya bhangi inayomkabili mwigizaji filamu, WemaSepetu (28) na wenzake wawili baada ya Jamhuri kudai mahakamani hapo kwamba upelelezi haujakamilika. “Leo (Jana) kesi hii ilitakiwa kufutiliwa mbali, ‘unasemaje tukapige chini, kwa nini unasema tusikapige chini,” alisema Hakimu Simba akimwambia wakili wa Serikali. Hakimuhuyoalitishiakuifutakesi hiyo akidaisababukuwaupelelezi wake haujakamilikakwa […]