Category: Burudani

NEY WA MITEGO ATEMA CHECHE

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘ Ney wa Mitego’, amewaonya wasanii wanaoendekeza matukio (kiki) badala ya kufanya kazi nzuri zitakazokubalika, waache kufanya hivyo kwani wanaua muziki wa kweli. Ney wa Mitego ambaye hivi sasa yupo kwenye maandalizi ya Tamasha la Nguvu ya Kitaa litakalofanyika Jumamosi hii kwenye viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, jijiji Dar es Salaam, […]

MSHAIRI WA TANZANIA AMGUSA RAIS WA URUSI

NA MWANDISHI WETU RAIS wa Urusi, Vladimir Putin, mwishoni mwa wiki iliyopita aliguswa na mashairi mazuri kutoka kwa msanii wa Ushahiri wa Tanzania, Aisha King, katika hafla ya kufungua tamasha la vijana na wanafunzi lililofanyika jijini Sochi, nchini humo. Akizungumza mara baada ya kukabidhi ushairi huo kwa Rais Vladimir Putin, Aisha alitunga mashairi hayo kwa maalumu ya kumshukuru kiongozi huyo […]

BEATRICE KITAULI ANG’AA TUZO ZA XTREEM KENYA

NA CHRISTOPHER MSEKENA TUZO maarufu za muziki wa Injili nchini Kenya, Xtreem Awards 2017, zimetangaza majina ya waimbaji wa Afrika wanaowania vipengele mbalimbali, ambapo Tanzania inawakilishwa na mwimbaji, Beatrice Kitauli aliyechomoza kwenye vipengele viwili. Akizungumza na Papaso la Burudani, Kitauli alisema nguvu ya mashabiki imefanya aibuke kwenye vipengele viwili ambavyo ni Kolabo Bora ya Mwaka na Mwimbaji Bora Tanzania. “Naomba […]

LOLA OMOTAYO; MWANAMKE ANAYETAJWA KUIVUNJA P SQUARE

LAGOS, Nigeria HABARI za kuvunjika kwa Kundi la P Square linaloundwa na mapacha Peter na Paul, si ngeni tena ingawa ziliwashangaza wadau wengi wa muziki barani Afrika. Kwa ubora wa tungo zake, kundi hilo liliweza kujizolea umaarufu mkubwa hata kwenye soko la tasnia ya burudani la kimataifa. Mfano mzuri ukiwa ni kufikia hatua ya kufanya kazi na staa wa hip […]

DOGO JANJA KUMUOA IRENE UWOYA… NI FILAMU AU KIKI

  NA JESSCA NANGAWE UKIACHANA na harusi ya mchekeshaji Lucas Mhaville ‘Joti’ aliyofunga mwishoni mwa wiki iliyopita, tetesi za msanii wa Bongo Fleva, AbdulAzizi Chande ‘Dogo Janja’ kudaiwa kufunga ndoa na Irene Uwoya, ndio imekuwa habari ya mjini kwa sasa. Maswali mengi yamebaki kwa mashabiki wa muziki na Bongo Movie wakishindwa kuelewa kama kuna ukweli wowote juu ya hilo, huku […]

HATA TYSON ANGECHAPWA NA AJ

  LOS ANGELES, Marekani MKONGWE wa masumbwi, Larry Holmes, amesema makali aliyonayo Anthony Joshua ‘AJ’ ulingoni kwa sasa yangetosha kummaliza hata aliyekuwa bingwa wa uzito wa juu duniani, Mike ‘Iron’ Tyson. Holmes amekuwa shabiki mkubwa wa AJ, ambaye ndiye anayeshikilia mikanda ya WBA na IBF. Nguli huyo anamfahamu vizuri Tyson, kwani ndiye aliyekomesha rekodi yake ya kushinda mapambano 38 mwaka […]

MWANA FA, AY WASHINDA TENA KESI YA MADAI

  NA MWANDISHI WETU MASTAA wa Bongo Fleva, Hamis Mwinjuma ‘Mwana Fa’ na Ambwene Yessaya ‘AY’, wamepata ushindi mwingine dhidi ya kesi yao ya madai na kampuni ya mawasiliano ya Tigo, ambayo Julai 21, mwaka huu, Mahakama Kuu ya Tanzania iliiamuru kampuni hiyo iwalipe wasanii hao Sh bilioni 2.1 kwa kutumia nyimbo zao (Usije Mjini, Dakika Moja) bila ruhusa. Baada […]

WASTARA KUZINDUA FILAMU ULAYA

  NA KYALAA SEHEYE MKALI wa filamu za kibongo, Wastara Juma, amesema baada ya kuzindua filamu yake ya Kibwebwe hapa nchini, hivi sasa anatarajia kusafiri kwenye kuizindua nchini Uingereza na Sweden, ambako nako ana mashabiki wengi. Wastara ameliambia Papaso la Burudani kuwa, Kibwewe ni filamu yenye uhalisia wa mwanamke wa Kitanzania, huku ikiwa imebeba ujumbe kwa watu wote duniani, ndiyo […]

R. KELLY KAZI ANAYO UNAAMBIWA

LAGOS, Marekani MAMBO si mazuri kwa upande wa mwanamuziki R. Kelly, ambapo mwanamke mwingine ameibuka na kusema aliwahi kumtesa. Hii si mara ya kwanza kwa R. Kelly kukutwa na kashfa hiyo kwani tayari kuna orodha ndefu ya wanawake waliowahi kumshutumu. Mwanamke huyo aitwaye Kitti Jones, alisema aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii huyo zaidi ya miaka miwili iliyopita. […]