Category: Burudani

DITTO:KUTOKA WATUPORI, LA FAMILIA HADI THT

  NA GLORY MLAY MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Lameck Ditto ‘Ditto’, aliibuliwa na msanii mkongwe, Seleman Msindi ‘Afande Sele’, mwaka 2003 katika tamasha la kuibua vijana wadogo wenye vipaji lililoandaliwa na kituo cha Redio Ukweli kilichokuwa na makazi yake mkoani Morogoro. Kipindi hicho akiitwa Dogo Ditto, alishirikishwa kwenye nyimbo zote za albamu ya pili ya Afande Sele iliyokwenda […]

KUTOKA VIDEO QUEEN HADI KUINGIA STUDIO, KUIGIZA

  NA MAREGES NYAMAKA KUNA msemo wa mitaani usemao ‘hupaswi kuridhika na kazi moja kama chanuo la nywele, kama inatokea mbele yako kuna fursa itumie.’ Msemo huo umeonekana kuwa na maana kubwa sana. Kama ilivyo katika medani nyingine, kwa siku za hivi karibuni msemo huo unaonekana kuwatokea wengi katika sanaa nchini. Tumeona jinsi vijana wengi walivyoamua ‘kuchangamkia tenda’ kwa kuhama […]

KISA CHA YAMOTO BAND KUVUNJIKA KIMYA KIMYA-4 Marombosso afunguka

  NA TIMA SIKILO WASANII wa Yamoto Band wamekuwa wakijitetea na kusisitiza kwamba kundi lao halijavunjika na bado wako pamoja, lakini kuna dalili za wazi zinaonyesha kwamba Yamoto Band imevunjika kimya kimya na ndiyo maana kila mmoja ameendelea kutoa kazi zake binafsi. Mpaka sasa waimbaji wa bendi hiyo kama Enock Bella na Bela Flavor wameshatoa nyimbo zao kila mmoja, huku […]

MSAFIRI ZAWOSE ATOA SIRI YA WAZUNGU KUUPENDA MUZIKI WA ASILI

INATOKEA mara chache sana hapa Bongo kwa msanii wa muziki wa asili kupata nafasi ya kushiriki kwenye tuzo kubwa za kimataifa, tumezoea kuona wakali wa Bongo Fleva kama vile Ali Kiba, Diamond Platnumz, Vanessa Mdee na wengineo wakituwakilisha vyema huko ugenini. Kwa maana hiyo tunapoona msanii wa muziki wa asili amepata nafasi ya kuliwakilisha Taifa kwenye kinyang’anyiro chochote kile hatuna […]

BIEBER AKATAA UBAGUZI WA RANGI

LOS ANGELES, Marekani LICHA ya vituko vyake, mwanamuziki wa pop, Justin Bierber, ameonesha kutounga mkono ubaguzi wa rangi unaoendelea nchini Marekani dhidi ya raia wenye asili ya Afrika. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23, amesema atafanya anachokiweza kukomesha tabia hiyo ili kuhakikisha usawa unapatikana. Bierber alitumia akaunti yake ya mtandao wa Instagram kuunga mkono  kampeni ya kupinga matukio ya […]

DAH! ETI P-SQUARE IMEVUNJIKA

LAGOS, Nigeria IMERIPOTIWA kuwa kundi la muziki la P-Square, linaloundwa na mapacha Paul na Peter Okoye limevunjika na huenda ukawa ndio mwisho wa uhondo wa kuwaona wawili hao wakiwa pamoja jukwaani. Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, Peter ndiye aliyeamua kuondoka kwenye kundi hilo lenye umaarufu mkubwa kweye soko la muziki barani Afrika. Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari, Peter anatajwa kukerwa […]

DIAMOND AMFUATA ZARI AFRIKA KUSINI, WAPEANA MAHABA

NA CHRISTOPHER MSEKENA BAADA ya kukiri kuchepuka na mwanamitindo, Hamisa Mobetto, kwenye uhusiano wake imara na Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’, msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amemfuata mama watoto wake Afrika Kusini na kumwomba msamaha. Katika kile kinachoonekana kuwa Zari The Boss Lady amemsamehe Diamond Platnumz na kumpa ruhusa ya kujumuika naye kwenye sherehe yake ya […]

HAPA KIBA, KULE FID Q HAPATOSHI FIESTA MWANZA LEO

NA MWANDISHI WETU UWANJA wa CCM Kirumba, jijini Mwanza, unatarajiwa kuwaka moto kesho wakati wasanii wakali wa hapa nchini, wakiongozwa na Ali Kiba, Fid Q, Roma Mkatoliki, Joh Makini, Ben Pol na Nandy, watakapopanda jukwaani kufanya vitu vyao katika tamasha la Tigo Fiesta 2017. Wasanii wengine ni Jux, Maua, Weusi, Rayvanny, Aslay, Young Killer, Rosa Ree, Lulu Diva, Darasa, Rostam, […]

JOKATE: KWA YANGA HII, NDANDA ITACHEZEA SABA

RAUNDI ya nne ya Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea wikiendi hii, ikiwa ni baada ya kuanza juzi Alhamisi kwa mchezo mmoja kati ya Simba na Mbao FC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza. Gazeti lako pendwa la michezo, BINGWA, linakuletea safu mpya ambapo mwandishi wetu mwandamizi katika kuripoti habari za soka na mfuatiliaji mzuri wa mechi na timu […]

JOKATE: KWA YANGA HII, NDANDA ITACHEZEA SABA

RAUNDI ya nne ya Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea wikiendi hii, ikiwa ni baada ya kuanza juzi Alhamisi kwa mchezo mmoja kati ya Simba na Mbao FC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza. Gazeti lako pendwa la michezo, BINGWA, linakuletea safu mpya ambapo mwandishi wetu mwandamizi katika kuripoti habari za soka na mfuatiliaji mzuri wa mechi na timu […]