Category: Burudani

JIKE SHUPA ARUDI KUUZA CHAKULA

NA JEREMIA ERNEST (DSJ) MREMBO aliyejizolea umaarufu baada ya kuonekana kwenye video ya msanii, Nuh Mziwanda, Zena Abdallah ‘Jike Shupa’, ameamua kurudia kazi yake ya zamani ya kuuza chakula na kukisambaza kwenye ofisi mbalimbali za jijini Dar es Salaam. Akizungumza na Papaso la Burudani, Jike Shupa, alisema ameamua kufanya uamuzi huo ili kujiongezea kipato na kuondokana na utegemezi wa kutegemea […]

ODAMA KUZINDUA FILAMU KITOFAUTI

NA JEREMIA ERNEST (DSJ) STAA wa filamu za kibongo, Jennifer Kyaka ‘Odama’, leo anatarajia kuzindua filamu yake inayoitwa Mr Kiongozi kitofauti, kupitia mfumo mpya wa Kampuni ya Maxicom Africa (Maxi Malipo), utakaowezesha kusambaza kazi kwa urahisi. Akizungumza na Papaso la Burudani, Odama alisema mfumo huo una lengo la kuinua kazi za sanaa kwa kurahisisha usambazaji kutoka kiwandani mpaka kuwafikia walaji, […]

SNURA AAHIDI KURUDI TENA KIBITI

NA KYALAA SEHEYE MAPOKEZI makubwa aliyoyapata msanii wa Bongo Fleva, Snura katika Wilaya ya Kibiti, mkoani Pwani, katika kampeni ya kuelimisha madhara ya unywaji dawa kiholela, staa huyo ameahidi kurudi tena wilayani humo. Akizungumza na Papaso la Burudani, Snura alisema mapokezi hayo makubwa yalimfanya atoe machozi ya furaha na kuahidi kurudi tena Kibiti na kudondosha shoo ya bure. “Kwa kweli […]

 DIAMOND AMNASA ‘MCHAWI’ WA VIOLIN

NA CHRISTOPHER MSEKENA KUPITIA albamu yake ya kimataifa inayoitwa A Boy From Tandale, msanii Abdul Naseeb ‘Diamond Platnumz’ amefanikiwa kumnasa na kumshirikisha mcheza ‘violin’ maarufu raia wa Israel na Marekani, Miri Ben Ari, katika wimbo wa Baila, utakaopatikana kwenye albamu hiyo.  Mrembo huyo mshindi wa tuzo kubwa ya Grammy, ambaye aliwahi kuitwa kutumbuiza Ikulu ya Marekani na Rais mstaafu Barack […]

BABU SEYA ‘OUT’, MASTAA WAZUNGUMZA

NA CHRISTOPHER MSEKENA BAADA ya kifungo cha miaka 13 jela,  ndoto ya wanamuziki Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanawe, Johnson Nguza ‘Papi Kocha’ kurudi uraiani imetimia mara baada ya Rais Dk. John Magufuli, kutangaza msamaha kwao katika maadhimisho ya 56 ya Uhuru wa Tanganyika yaliyofanyika juzi mkoani Dodoma. Juni 25 mwaka 2004, mastaa hao wa singo ya Tutoke Wote, walitiwa […]

SAHAR ANAWEZA KUFARIKI BAADA YA KUPASULIWA SURA MARA 50 AFANANE NA ANGELINA JOLIE

Tehran, Iran MREMBO mmoja wa nchini Iran, Sahar Tabar, aliyedaiwa kufanyiwa upasuaji wa sura mara  50 akitaka afanane na nyota wa filamu nchini Marekani, Angelina Jolie, amedaiwa kuwa anaweza kufariki dunia kutokana na njaa. Sahar, mwenye miaka 19, kutoka mjini Tehran, ambaye anadaiwa kuwa shabiki mkubwa wa mwigizaji huyo aliyecheza filamu ya Tomb Raider, aliweka picha zake kwenye mtandao wa […]

LIL WAYNE MBIONI KUIACHIA ‘DEDICATION 6’

NEW YORK, Marekani MKALI wa hip hop, Lil Wayne, amewatonya mashabiki wake kuwa hivi karibuni atawatupia albamu yake ya ‘Dedication 6’. Lila Wayne aliwaambia mashabiki wake kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram na wengi wao walionesha furaha isiyo ya kifani. “Nafurahi kuona mashabiki wangu wakinivumilia katika muda wote huu wa kupambana na hii kazi. Nisiwapotezee muda wenu, mzigo unashuka hivi […]

ADELE HANA WIMBO MIAKA MIWILI NA MPUNGA UNAINGIA

LONDON, England MWANAMUZIKI wa England, Adele, ameripotiwa kuvuna kiasi cha pauni milioni tisa kwa mwaka licha ya kutokuwa na wimbo mpya tangu 2015. Mkali huyo mwenye sauti maridhawa, mwenye albamu tatu zinazotamba pamoja na tuzo 15 za Grammy’s, anaonekana kupokea kiasi kikubwa cha fedha kwa mwaka licha ya kwamba hana kazi kubwa aliyoifanya ndani ya miaka miwili zaidi ya kulea […]

‘JANUARY TO DECEMBER’ YA HEMEDY PHD FUNGA MWAKA

  NA SHARIFA MMASI MSANII wa filamu na muziki nchini, Hemed Suleiman ‘Hemedy PhD’, amesema mapokezi makubwa ya wimbo wake mpya, ‘January To December’ yamefanya kazi hiyo iwe ya mwisho kwake mwaka huu. Hemedy PHD, alisema wimbo huo ambao ameutoa siku tatu zilizopita umepokewa vizuri kiasi cha kuimbwa na watu mbalimbali hata watoto kwenye mitaa mbalimbali. “January To December’ ni […]

DULLY SYKES AFUNGUKA ‘BOMBARDIER’ ILIVYOFANYIKA

  NA CHRISTOPHER MSEKENA MKONGWE wa muziki wa Bongo Fleva, Dully Sykes, amesema wimbo wake mpya, Bombardier aliyoiachia hivi karibuni ilifanyika ndani ya siku saba mpaka kukamilika. Akizungumza na Papaso la Burudani, Dully Sykes, licha ya kuogopa kupanda ndege, ndani ya wimbo huo amejifananisha na ndege hizo aina ya Bombardier zenye uwezo wa kuruka juu umbali mrefu na kukaa angani […]