Category: Burudani

TYSON FURY AMRUSHIA KIJEMBE TONY BELLEW

LONDON,  England   BONDIA Tyson Fury amesema kwamba licha ya hasimu wake,  Tony Bellew, kuibuka na ushindi katika raundi ya tano  dhidi ya mpinzani wake, David Haye, hawezi kumpiga na akatamba kuwa anaweza kumchakaza  bingwa huyo wa zamani wa  WBC hata kama atakuwa amefungwa mikono yake miwili nyuma.                     Taarifa hizo zinaonekana kuwa nzuri kwa Bellew mwenye rekodi ya (30-2-1, […]

SIMBA WAFUATA BARAKA ZA WABUNGE WAO *WAKITOKA DODOMA, KUIVAMIA SINGIDA UNITED KUMALIZA KAZI VPL

  NA ZAITUNI KIBWANA     KIKOSI cha Simba kinatarajiwa kuondoka Dar es Salaam kesho kwenda mkoani Singida tayari kwa mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Singida United, huku wakipanga kuweka vituo katika mikoa ya Morogoro na Dodoma. Singida United ambao ndio mwenyeji wa mchezo huo, watawakaribisha Simba kwenye Uwanja wa Namfua, mjini humo Jumapili, huku Wekundu […]

ZILIFIKAJE, ZIMEJIPANGAJE?

MOSCOW, Urusi   ZIMEBAKI siku kadhaa kabla ya kuanza kwa michuano ya fainali za Kombe la Dunia, zitakazofanyika nchini Urusi huku mataifa 32 yakishindana kuwania medali hizo pindi timu zao zitakapotinga fainali. Kila timu imetinga katika fainali hizo baada ya kucheza michezo kadhaa ambayo walifanikiwa kupata ushindi na hatimaye kukata tiketi ya kushiriki. Makala haya yanakuletea jinsi timu ya Ureno […]

UJIO WA KEITA, KICHEKO KWA KLOPP

MERSEYSIDE, England   KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp, amesema kuwa usajili wa kwanza wa kiungo mahiri wa RB Leipzig, Naby Keita, utakiboresha zaidi kikosi chake msimu ujao, pamoja na wachezaji kadhaa anaotarajia kuwaongeza. Keita anatarajiwa kutua Ligi Kuu England msimu ujao akitokea katika timu hiyo ya Bundesliga, baada ya Liverpool kukubaliana na Leipzig kuhusu uhamisho wa nahodha huyo wa timu […]

FAINALI MABINGWA ULAYA… BIL 42/- ZITAKAVYOWATOA JASHO MASTAA LIVER, MADRID

  LONDON, England     USIKU wa Mei 26 utakuwa wa burudani ya kukata na shoka kwa mashabiki wa kandanda ulimwenguni kote, siku ambayo Real Madrid watakipiga na Liver katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Ikumbukwe kuwa, mechi hiyo ndiyo itakayohitimisha msimu huu wa 63 wa mashindano hayo ya Shirikisho la Soka la Ulaya (Uefa). Liver hawajashiriki […]

YANGA YAPIGWA 4-0 NA USM ALGER

NA MWANDISHI WETU   WAWAKILISHI  wa Tanzania katika michuano ya kimataifa, Yanga wamechapwa kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya USM Alger ya Algeria katika mchezo wao wa kwanza wa Kombe la Kombe la Shirikisho Afrika. Mchezo huo wa Kundi D uliofanyika jana kuanzia saa 4:00 usiku kwenye Uwanja wa Omar Hammadi uliopo Bologhine mjini Algiers, Algeria, huku Yanga wakicheza mchezo […]

WENGER AAGWA VIZURI, CHELSEA YAIUA LIVER

LONDON, England   KLABU ya Arsenal jana imeibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya Burnley katika mchezo wa mwisho kwa kocha wao, Arsene Wenger, kuiongoza timu hiyo kwenye dimba la Emirates. Mtanange huo wa Ligi Kuu England, ulikuwa ni mmoja wa michezo iliyopigwa jana jioni, na kuwashuhudia washika mitutu hao wa London wakiitandika Burnley bila huruma. Wenger alikiongoza […]