Category: Burudani

TID: Sina tatizo na Lulu Diva, nipo tayari kumpa mtoto

NA MWANDISHI WETU MKALI wa Bongo Fleva, Khalid Mohamed ‘TID’, amesema hana tatizo na msanii Lulu Diva, baada ya kukaririwa akimtuhumu mrembo huyo kuwa amezaa na anamficha mtoto wake. Akizungumzia ishu hiyo jana kwenye kipindi cha XXL ya Clouds Fm, TID, alisema kuna mwandishi alimuuliza nini maoni yake kuhusu Lulu Diva ambaye ana mtoto na anamficha.  “Mimi sina tatizo na […]

Diamond, baba yake mambo poa, Zari akana kuchepuka

NA CHRISTOPHER MSEKENA HATIMAYE staa wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, amemaliza tofauti alizokuwanazo na baba yake mzazi, Abdul Juma ambaye hakuwahi kuonana naye kwa miaka 20 zaidi ya kuwasiliana kwenye simu. Hatua hiyo ilikuja baada ya wawili hao kukutanishwa kwa ‘surprise’ katika Studio za Wasafi Fm, ambapo Diamond Platnumz alikwenda kuzindua kipindi cha Block 89 na kuzungumza mambo […]

Hammer Q: Sijatusua, bado naudai muziki

NA JEREMIA ERNEST ZIPO nyingi ila ‘Pembe la Ng’ombe’ akiwa na Bendi ya Dar Modern Taarab, ndiyo ngoma iliyothibitisha kuwa si tu Bongo Fleva, hata muziki huo wa mwambao anauweza. Huyo si mwingine, ni Hussein Mohamed ‘Hammer Q’, ambaye alitamba zaidi katika miaka ya 2000, akitumia ngoma ya ‘Lady’ kujitambulisha Bongo Fleva. Kipindi hicho jamaa alikuwa chini ya lebo ya […]

Wizara izikumbuke sanaa za ufundi na ubunifu

NA CHRISTOPHER MSEKENA HIVI karibuni hotuba ya makadirio ya bajeti ya mwaka 2019/20 ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ilisomwa bungeni jijini Dodoma na Waziri Dk. Harrison Mwakyembe. Miongoni mwa mambo yaliyoibuka katika hotuba hiyo ni wasanii marehemu kama Steven Kanumba na Mzee Majuto kulipwa fedha zao za fidia baada ya upitiaji upya wa mikataba ya kazi walizowahi […]

Lulu Diva, Wakazi hapatoshi Kigamboni mkesha wa Pasaka

NA MWANDISHI WETU KATIKA kusherehekea mkesha wa Sikukuu ya Pasaka, mamia ya mashabiki wa Bongo Fleva wanaoishi Kigamboni, Dar es Salaam, wanatarajia kupata burudani ya nguvu kutoka kwa Lulu Diva na rapa Wakazi. Mratibu wa onyesho hilo, Mbwana Khamis, alisema wasanii hao watadondosha burudani katika klabu ya usiku ya Jembe One kuanzia saa mbili usiku na kuendelea. “Mbali na Lulu […]

Kampuni zilizoiingia mikataba na Kanumba, Majuto kuzilipa familia zao

Mwandishi Wetu Kampuni ya Steps Entertainment imeshamkabidhi Mama wa  muigizaji marehemu, Steven Kanumba malipo ya ziada ya Sh milioni 15 baada ya kugundulika kuwa iliingia mkataba mbovu na msanii huyo. Pia kampuni hiyo imeahidi kushirikiana na mama yake Marehemu Kanumba, kuandaa filamu ya maisha ya mwanawe huyo. Taarifa hiyo ilitolewa bungeni leo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, […]

Lulu: Hakuna ninachojutia kwenye maisha yangu

NA MWANDISHI WETU MWIGIZAJI nyota nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’, amesema hakuna jambo  lolote analojutia kwenye maisha yake kwa kuwa yamemjenga na kuwa imara kama alivyo sasa. Akizungumza jana na kipindi cha XXL ya Clouds Fm, Lulu alisema anaamini katika mambo mazuri na mabaya aliyoyafanya yamekuwa na mchango mkubwa kwenye maisha yake ya sasa. “Kiukweli hakuna ninachojutia kwenye maisha yangu, sababu […]

WANATOKA

W*Solskjaer apanga kufanya maajabu Camp Nou, kocha Barca ampiga kijembe *Ajax ‘full’ mzuka unaambiwa, Juve kukomaa mwanzo-mwisho CATALUNYA, Hispania USIKU wa Ulaya umerejea tena, moto ni uleule katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa vigogo wa nchini England, Manchester United, kushuka uwanjani leo watakapokuwa wageni wa Barcelona. Wiki iliyopita timu hizo zilipokutana, Barcelona walifanikiwa kushinda bao 1-0 […]

Khadija Yusuph arudi kundini kuokoa Jahazi

NA JEREMIA ERNEST MWANAMUZIKI nyota wa taarabu nchini, Khadija Yusuph, ameamua kurudi tena katika bendi pendwa ya muziki huo, Jahazi Modern Taarab ili kuiweka tena kwenye ramani kama ilivyokuwa zamani. Akizungumza na Papaso la Burudani jana, Khadija alisema anarudi kundini kuiokoa bendi ya Jahazi ambayo imekuwa ikishuka kadiri siku zinavyokwenda toka mwasisi wake Mzee Yusuph aache muziki. “Tumerudi katika bendi […]

Jay Z aunda mfuko kusaidia familia ya Nipsey

LOS ANGELES RAPA Shawn Carter, maarufu kama Jay Z, ameunda mfuko ambao atachangia kiasi cha dola za Marekani milioni 15, ambazo ni zaidi ya Sh bilioni 34.7 kwaajili ya kusaidia watoto wa marehemu Nipsey Hussle, aliyefariki dunia wiki hii kwa kupigwa risasi huko Los Angeles, Marekani. Jay Z, ambaye alimsaini Nipsey katika lebo yake ya Roc Nation, ameweka wazi kuwa […]