Category: Burudani

Nandy Festival hapatoshi Kahama

NA SICSA MACHABA BAADA ya kufanya vizuri mkoani Tanga, tamasha la Nandy Festival, leo linatarajiwa kuwasha moto wa burudani kwa mashabiki wa Mji wa Kahama ndani ya Uwanja wa Taifa. Nandy, ameliambia Papaso la Burudani kuwa maandalizi yamekamilika na leo ataongoza wasanii kama Rostam (Roma na Stamina), Marioo na Dogo Janja, kuwapa burudani mashabiki mjini huko kabla ya kesho kuhamia […]

R.Kelly adhoofika akiwa jela

CHICAGO, Marekani STEVE Green ambaye ni mwanasheria anayesimamia kesi zinazomkabili mfalme wa muziki wa RnB duniani, Robert Kelly, amevijuza vyombo vya habari nchini Marekani kuwa afya ya staa huyo akiwa rumande imedhoofika. Imeripotiwa kuwa R. Kelly, anayetuhumiwa kuwanyanyasa kingono wasichana wadogo, ameendelea kupitia wakati mgumu kwani amepoteza uwezo wa kuona vizuri jambo linalompa shida kusoma barua pepe anazotumiwa na Biblia […]

Aussems atoa msimamo, aitaja Azam

NA WINFRIDA MTOI KUELEKEA mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC, Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, amesema katika mchezo huo ataingia na kikosi tofauti na kile kilichoivaa UD Songo. Simba inatarajia kukabiliana na Azam FC katika mchezo huo, ukataopigwa keshokutwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Wekundu wa Msimbazi hao, watacheza mchezo huo, huku wakifikiria […]

Zahera atumia video kuiua Township Rollers

NA WINFRIDA MTOI BAADA ya kushindwa kutamba nyumbani, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, ameamua kutumia mbinu nyingine kuandaa kikosi cha maangamizi kuelekea mchezo wao wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers ya Botswana. Yanga walitoka sare ya bao 1-1 na Rollers katika mchezo wa kwanza wa michuano hiyo wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar […]

Gadiel akiona cha moto Simba

LOVENESS BERNARD Beki wa kushoto wa Simba, Gadiel Michael, amekiona cha moto baada ya kufanyiwa ‘kitu mbaya’ na mshambuliaji tishio wa timu hiyo, asiye na urafiki na makipa wa timu pinzani, Meddie Kagere. Gadiel yalimkuta hayo wakati wa mazoezi yaliyofanyika juzi jioni kwenye Uwanja wa Gymkhana, Dar es Salaam, ikiwa ni maandalizi ya mchezo wa Ngao ya Jamii, utakaopigwa Jumamosi […]

U-15 fiti kushiriki Cecafa

GLORY MLAY Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri chini ya miaka15 ( U-15),  Maalim Saleh, amesema  wachezaji wake wameiva kwa michuano ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika, Mashariki na Kati (Cecafa). Michuano hiyo imepangwa kuanza Ijumaa hadi Septemba mosi, mwaka huu, nchini Eritrea. Akizungumza na BINGWA jana, Saleh alisema wachezaji wapo fiti kwa michuano […]

Ligi Daraja la Kwanza netiboli kufanyika Dodoma

HELLEN GERALD (TUDARCo) Ligi Daraja la Kwanza ya netiboli, imepangwa kufanyika jijini Dodoma, ikishirikisha timu 19 za wanawake na wanaume. Daraja la Kwanza ya netiboli, imepangwa kufanyika jijini Dodoma, ikishirikisha timu 19 za wanawake na wanaume. Akizungumza na BINGWA juzi, Katibu Mkuu wa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta),  Judith Ilunda, alisema ligi hiyo itaanza mwishoni mwa mwezi huu. “Tumejipanga vizuri […]

Caf yasogeza mbele mechi ya Simba, JKT Tanzania

WINFRIDA MTOI Mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Simba na JKT Tanzania, iliyokuwa imepangwa kuchezwa Agosti 23, imesogezwa mbele hadi Agosti 29, mwaka huu, kutokana na mwingiliano ya michuano ya Kimataifa. Kwa mujibu wa ratiba ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf), Simba watakuwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, kucheza na UD Songo ya Msumbuji katika mchezo […]