Category: Burudani

Wasanii Uzalendo Kwanza waonyeshwa viwanja vyao

NA BRIGHITER MASAKI KAMPUNI ya KC Land Development Plan imewapeleka wasanii wanaounda Chama cha Uzalendo Kwanza katika viwanja watakavyopewa vilivyopo eneo la Mwasonga, Kigamboni, jijini Dar es Salaam. Akizungumza na Papaso la Burudani juzi, Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza, Steve Nyerere, alisema anaishukuru kampuni hiyo kwa kuwafikiria wasanii na watu masikini katika kuwawezesha kwenye suala la kumiliki ardhi. “Wasanii tumekuwa tukitangatanga […]

Chuchu Hans akaribisha wadhamini Miss Tanga

NA JEREMIA ERNEST MWIGIZAJI wa filamu ambaye pia ni mwandaaji wa shindano la urembo, Miss Tanga, Chuchu Hans, amesema anakaribisha kampuni na taasisi mbalimbali zinazoweza kudhamini mashindano hayo. Akizungumza na Papaso la Burudani, Chuchu ambaye aliwahi kushiriki Miss Tanzania mwaka 2005 akiwakilisha Mkoa wa Tanga, mbali na kuhitaji wadhamini nafasi kwa warembo wenye vigezo, zipo wazi hivyo wajitokeze kuchukua fomu. […]

Mastaa waungana kumlilia Mengi

NA MWANDISHI WETU BAADA ya taarifa za kifo cha mfanyabiashara maarufu Afrika Mashariki, Dk. Reginald Mengi, mastaa mbalimbali wa muziki na filamu wameungana kutoa salamu za rambirambi kwa familia, ndugu na marafiki kama ifuatavyo. Diamond Platnumz: Dah! Hii habari mbaya, Mungu ailaze roho na nafasi yako ya unyenyekevu pema peponi. Vanessa Mdee: Poleni sana kwa ndugu jamaa na marafiki pamoja […]

Wasanii kunufaika na viwanja vya mkopo

Brighiter Masaki, Dar es Salam Kampuni ya KC Land Development Plan imepanga kuwapatia wasanii ambao ni wanachama wa kikundi cha Uzalendo Kwanza viwanja kwa mkopo ili waweze kumiliki ardhi na kujenga makazi. Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 2, Mwenyekiti wa kikundi hicho, Steve Magere maarufu Steve Nyerere amesema kampuni hiyo imefanya jambo kubwa na muhimu kwa wasanii. “Wasanii […]

Gofu kushiriki Zone 4 Burundi

NA GLORY MLAY TIMU ya Taifa ya gofu inajiandaa kushiriki michuano ya Zone 4 itakayofanyika Juni mwaka huu nchini Burundi. Akizungumza na BINGWA jana, kocha mkuu wa timu hiyo, Hassan Kadio, alisema wameanza maandalizi ya michuano hiyo. Kadio alisema tayari wamechagua wachezaji katika michuano iliyofanyika wiki iliyopita mjini Moshi   mkoani Kilimanjaro. Alisema katika michuano hiyo, walifanikiwa kuchagua wachezaji wanne ambao […]

Michuano ya kimataifa karate kufanyika Julai

NA MWANDISHI WETU TANZANIA inatarajiwa kuwa mwenyeji wa michuano ya kimataifa ya karate iliyopangwa  kufanyika Julai mwaka huu jijini Dar es Salaam, ikishirikisha Bara la Afrika na Asia. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwenye vyombo vya habari juzi na Mkufunzi Mkuu wa Karate Tawi la Tanzania, Jorome Mhagama, michuano hiyo imeandaliwa kwa lengo la kujenga urafiki na uhusiano. Taarifa hiyo […]

Gmifrak Master; Mkali wa ‘Free Style’ anayewatamani Rosa Ree, Chemical

NA CHRISTOPHER MSEKENA KARIBU tena katika safu hii ya Jiachie na Staa Wako, safu inayokukutanisha na watu maarufu kwenye sekta ya burudani ndani na nje ya Bongo na leo hii tupo na  George Michael ‘Gmifrak Master’, rapa ambaye alikuwa karibu zaidi na marehemu Godzilla aliyefariki miezi miwili iliyopita, karibu. SWALI: Emanuel Mwakyoso kutoka Mbeya, anauliza kwanini nguzo ya hip hop […]

Wasanii kuzindua albamu zao Kenya, wawekezaji Bongo mpo?

NA CHRISTOPHER MSEKENA MWISHONI mwa wiki katika klabu ya Golden Ice Bistro jijini Nairobi, Kenya, ulifanyika uzinduzi mkubwa wenye mafanikio wa albamu (santuri) ya kwanza ya staa wa Bongo Fleva, Faustine Charles ‘Nandy’. Santuli hiyo yenye jumla ya ngoma 13, imeendelea kuonyesha kuwa bado soko la muziki wa kizazi kipya linahitaji wasanii wake watoe albamu kwa kuwa mashabiki wa kuzinunua […]