Category: Burudani

Kwanini Serikali ya Ufaransa haitakubali Mbappe kuuzwa Madrid?

PARIS, Ufaransa KLABU ya Real Madrid imeweka wazi kwamba wanataka kutoa ofa ya kumnasa mshambuliaji wa PSG, Kylian Mbappe. Lakini timu hiyo ya PSG inategemea nguzo mbili zinazofanya iendelee vizuri, ambapo moja ni mchezaji huyo wa Ufaransa, Mbappe na nyingine ni Neymar. Mchezaji huyo wa zamani wa Monaco, aliwasili kwenye klabu hiyo ya Parc des Princes kama mchezaji ghali duniani […]

Pilipili kuongoza mashambulizi ‘Arusha Comedy Festival’ 

NA CHRISTOPHER MSEKENA MCHEKESHAJI bei mbaya kwa sasa Bongo, Emmanuel Mathias ‘MC Pilipili’, anatarajia kuongoza mashambulizi ya burudani jijini Arusha kwenye onyesho la Arusha Comedy Festival 2019, litakalofanyika Aprili 22, mwaka huu katika ukumbi wa Aim Mall. Pilipili, ambaye kabla ya onyesho hilo atakonga nyoyo za wakazi wa Dodoma katika onyesho lake la ‘Man From Swaswa’ kwenye sikukuu ya Pasaka, […]

Queen Elizabeth apata shavu la utalii

NA JEREMIAH ERNEST MREMBO aliyetwaa taji la Miss Tanzania 2018/19, Queen Elizabeth Makune, ametangazwa na Bodi ya Utalii nchini kuwa balozi wa vivutio vya utalii nchini kwa muda wa mwaka mmoja. Akizungumza na Papaso la Burudani wakati wa hafla ya kuweka saini ya mikataba ya dili hilo jijini Dar es Salaam jana, Queen alisema amefurahi kupata nafasi hiyo na atashirikiana […]

Maandilizi tamasha la AWAFFEST yakamilika

NA JEREMIA ERNEST BALOZI wa Tamasha la African Women Arts and Film (AWAFFEST) linaloandaliwa na The African Film Festival, Yvonne Cherry ‘Monalisa’, amesema tamasha hilo litafanyika Aprili 29 hadi 31, mwaka huu katika Makumbusho ya Taifa na Mlimani City, Dar es Salaam. Akizungumza na Papaso la Burudani, Monalisa alisema tamasha hilo litahusisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Nigeria, Ghana na […]

Kaka Jay aibuka na Matendo ya Mungu

NA MWANDISHI WETU BAADA ya kufanya vizuri na wimbo wa Tanzania unaosifia mambo mbalimbali mazuri yanayopatikana nchini, mwimbaji Joash Timoth Omolo ‘Kaka Jay’, ameachia video ya wimbo mpya wa Matendo ya Mungu. Kaka Jay ameliambia Papaso la Burudani kwamba, wimbo huo umelenga kuikumbusha dunia mambo mbalimbali ambayo Mungu amekuwa akiyafanya kwa binadamu wote, hivyo anaamini utawagusa watu wengi. “Kwenye Matendo […]

Like Shwary hakamatiki aisee

NA GLORY MLAY ISACK Luvanda maarufu kama Like Shwary ambaye ni rapa anayefanya vizuri jijini Mbeya, amesema anashukuru mashabiki kwa mapokezi makubwa ya video yake mpya ya My Property. Akizungumza na Papaso la Burudani jana, Like Shwary alisema toka mwaka ulipoanza alikuwa kimya akifanya maandalizi ya kazi zake mpya ambazo ameanza kuachia  moja moja. “My Property inafanya vizuri sana huko […]

Jokate kusaidia elimu ya mtoto wa kike

NA BRIGHER MASAKI MWANAMITINDO maarufu nchini ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, anatarajia kufanya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia watoto wa kike Machi 30, mwaka huu katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam. Akizungumza na Papaso la Burudani ambaye juzi alisherehekea siku yake ya kuzaliwa, Jokate alisema katika tafrija hiyo itaongozwa na Makamu […]

Koffi hatiani kwa kubaka, wanenguaji walia kunyanyaswa

NANTERRE, UFARANSA MAHAKAMA ya Nanterre nchini Ufaransa, imemhukumu mwanamuziki nyota Afrika, Koffi Olomide, kwenda jela miaka miwili huku mwenyewe akiwa kwao Kinshasa, Kongo, baada ya kumkuta na hatia ya kumbaka mnenguaji wake aliyekuwa na miaka 15 wakati huo. Uamuzi huo una maana kwamba Koffi atakamatwa iwapo atatekeleza uhalifu mwingine, huku mahakama ikimtaka alipe faini Euro 5,000, ambazo ni zaidi ya […]

R. Kelly akanusha kutoka na mkwewe

LOS ANGELES, Marekani HUKU akiwa na kesi 10 za unyanyasaji wa kingono, R. Kelly amegomea taarifa mpya kuwa aliwahi ‘kuchepuka’ na Diane Haughton, mama mzazi wa aliyekuwa mpenzi wake, Aaliyah. Si mwingine bali ni Lisa Van Allen, mmoja kati ya wanawake waliosema walinyanyaswa kingono na R. Kelly, ndiye aliyeibua madai hayo mapya. “(R. Kelly) alikuwa anaishi nyumbani kwao (ukweni) kule […]