Category: Burudani

Aunt Ezekiel adai mashabiki ni pasua kichwa

NA BEATRICE KAIZA, STAA wa filamu za Tanzania, Aunt Ezekiel, amedai kuwa mashabiki wengi ni pasua kichwa kwa kuwa ndio chanzo cha ugomvi unaotokea kati ya msanii mmoja na mwingine. Akizungumza na Papaso la Burudani, Aunt alisema ni ngumu kufanikiwa kwenye kazi bila nguvu ya mashabiki, ila mashabiki wa Tanzania ndio wamekuwa wakichangia kwa namna moja ama nyingine kuibomoa tasnia […]

Tatizo la Diamond ni Tandale, fedha au tuzo?

NA MICHAEL MAURUS, JUMANNE ya wiki iliyopita katika ukurasa huu, nilianza na mfululizo wa makala haya yanayohusiana na maisha ya msanii wa muziki wa kizazi kipya, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’. Katika makala hayo, nilielezea jinsi Diamond anavyochukiwa na baadhi ya wapenzi wa muziki hapa nchini pamoja na ukweli kwamba ndiye msanii mwenye mafanikio zaidi kwa kutwaa tuzo nyingi nje ya […]

WINNIE CUTE Mrembo wa Singida aliyetekwa na Diamond

NA MICHAEL MAURUS, UKIKUTANA naye kwa mara ya kwanza, unaweza kudhani ni mmoja wa washiriki wa mashindano ya urembo nchini ya Miss Tanzania kutokana na umbo lake. Ni binti mwenye mvuto wa aina yake, akiwa na tabasamu la hali ya juu, mcheshi na mzungumzaji pale inapobidi kufanya hivyo. Kwa mara ya kwanza kuonana naye, ni pale alipofika katika ofisi za […]

Mpenzi mpya wa Wema hamjui kabisa Idris

NA ZAITUNI KIBWANA, MWANAMITINDO anayedaiwa kuchukua nafasi ya Idris Sultan kwa kutoka kimapenzi na Wema Sepetu, ametoa kali ya mwaka kwa kusema kamwe hamtambui ‘ex’ wa mrembo huyo. Mwanamitindo huyo anayejulikana kwa jina la Calisah Abdulhamid, ametoa kali hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha FridayNite Live. “Idris ni nani, kwani amewahi kuwa mshindi wa  Big Brother? […]

AY, Dj D Ommy, Diamond, Harmonize wawafuta machozi Watanzania

NA HAPPYGLORY URASSA, BAADA ya nyota 6 wa Bongo Fleva kutoka kapa katika tuzo za MTV MAMAs 2016 zilizofanyika juzi, Johannesburg, Afrika Kusini, wasanii AY, Dj D-Ommy, Diamond Platnumz na Harmonize wameibuka washindi kwenye tuzo za African Entertainment Awards USA (AEAUSA), zilizotolewa usiku wa kuamikia jana huko New Jersey, Marekani. Kabla ya tuzo hizo kutolewa, juzi usiku mastaa wa Bongo […]

Kajala amtabiria makubwa mwanawe

NA KYALAA SEHEYE, KUFUATIA maisha ya shida yenye mikasa mingi ya hatari aliyowahi kuishi nyota wa filamu za Kitanzania, Kajala Masanja, msanii huyo amesema hayupo tayari kuona mwanawe Paula anaishi kama yeye. Kajala ameliambia Papaso la Burudani kuwa hapendi mtoto wake huyo wa kike awe msanii ila anatamani aje kuwa mtu mkubwa mwenye mamlaka ya nchi hii ndiyo maana anatafuta […]

Nandy humwambii kitu kwa Mwasiti

NA BEATRICE KAIZA, BAADA ya kufanya kava ya Nalivua Pendo wimbo ulioimbwa na msanii Mwasiti miaka kadhaa iliyopita, staa wa singo ya Nagusa gusa, Faustina Mfinanga ‘Nandy’, amesema yeye ni shabiki namba moja wa mwanamuziki huyo. Nady ambaye aliwahi kuiwakilisha vyema Tanzania kwenye shindano ya Tecno Own The Stage, ameliambia Papaso la Burudani kuwa ameamua kufanya kava ya wimbo huo […]

Hiki ndicho kinachomponza Diamond Platnumz

NA MICHAEL MAURUS, DAKIKA kama si saa chache baada ya msanii wa muziki wa kizazi kipya wa Tanzania, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ kutwaa Tuzo ya Afrimma 2016, kupitia kipengele cha Msanii Bora wa Kiume Afrika Mashariki, wadau wa muziki na wengineo hapa nchini, haraka mno walianza kutoa maoni yao kupitia njia mbalimbali, zaidi ikiwa ni mitandao ya kijamii. Hafla ya […]

Kim Kardashian arejea nyumbani kimya kimya

LOS ANGELS, Marekani STAA Kim Kardashian, amenaswa akirejea kimya kimya nyumbani kwake jijini  Los Angeles, ikiwa ni takribani wiki moja tangu aporwe na vibaka mjini Paris nchini Ufaransa. Mwanamama huyo mwenye umri wa miaka 35, alinaswa mwishoni mwa wiki wakati akienda kula chakula cha usiku huku amevalia nguo ndefu nyeusi zilizomfunika hata kichwani na kubakiza sura yake tu. Vyanzo vya […]

Linah adai hajutii kukosa tuzo ya Afrimma

NA BEATRICE KAIZA, BAADA ya kukosa tuzo ya Afrimma iliyotolewa mwishoni mwa wiki iliyopita huko Dallas, Texas nchini Marekani, Esterina Sanga ‘Linah’, amesema hajutii kuikosa tuzo hiyo kwani imemwongezea kasi ya kufanya kazi nzuri zaidi. Linah aliyekuwa anawania tuzo kwenye kipengele cha Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki, tuzo iliyochukuliwa na Akothee kutoka nchini Kenya, ameliambia Papaso la Burudani kuwa […]