Category: Burudani

Conte aishangaa Inter Milan kuchelewesha dili la Lukaku

MILAN, Italia INTER Milan wamepata ubaridi, baada ya kuambiwa walipe pauni milioni 75 ili waweze kupata saini ya straika wa Manchester United, Romelu Lukaku. Suala hilo linaonekana kumchosha kocha wa Inter Milan, Antonio Conte ambaye alimfanya Lukaku chaguo la kwanza kusajiliwa ndani ya kikosi hicho cha mabingwa wa zamani wa Italia. Hivi sasa straika huyo yupo nchini Singapore na kikosi […]

Ngassa anukia unahodha Yanga

MICHAEL MAURUS BAADA ya Ibrahim Ajib kuondoka Yanga, kitambaa cha unahodha ndani ya timu hiyo kwa sasa kipo wazi kwa wachezaji watatu, miongoni mwao, akiwa ni winga machachari, Mrisho Ngassa. Ajib aliyetimkia Simba baada ya mkataba wake Jangwani kumalizika, alipewa cheo hicho kutoka kwa Kelvin Yondani, huku msaidizi wake, akiwa ni Juma Abdul. Lakini wakati nafasi kubwa ya unahodha ikionekana […]

Kaseja ajifua kivyake kumkabili Manula Stars

ZAINAB IDDY KIPA Juma Kaseja ameendelea kujifua kivyake, licha ya kocha wa timu yake ya KMC,  Jackson Mayanja,  kuwapa mapumziko ya siku tatu, baada ya kurejea nchini wakitokea Kigali, Rwanda kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu Kombe la Kagame. KMC iliyoshiriki kwa mara ya kwanza michuano ya Kagame ilishindwa kutinga robo fainali kutokana na kufanya vibaya […]

Uwoya, Barnaba kuipamba Miss Moro

MICHAEL MAURUS, MOROGORO MSANII mahiri wa filamu, Irene Uwoya na mkali wa Bongo Fleva, Barnaba, wanatarajiwa kupamba kinyang’anyiro cha Miss Morogoro 2019, kwenye ukumbi wa Morogoro Hoteli, mjini hapa leo, huku kukiwa na shoo kali kutoka kwa mkali wa muziki wa dansi, Christian Bella. Kwa mujibu wa mratibu wa shindano hilo, Farida Kulususu, jumla ya warembo 12 watapanda jukwaani kuwania […]

Dkt. Msolla aja na mkakati kabambe

MICHAEL MAURUS, MOROGORO MWENYEKITI wa Yanga, Dkt. Mshindo Msolla, amepanga kukutana na mchezaji mmoja mmoja ili kuwaweka sawa kabla ya kuanza kwa msimu ujao, wakikabiliwa na michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika. Akizungumza na BINGWA jana alipotembelea mazoezi ya timu hiyo ya asubuhi yaliyoambatana na mechi ya kirafiki dhidi ya Moro Kids, kwenye Uwanja wa […]

Vita yaanza Simba

WINFRIDA MTOI BAADA ya kukamilika kwa kikosi cha Simba katika kambi yao iliyopo Afrika Kusini, mchuano wa kugombea namba umeanza kuwa mkali, hasa wa washambuliaji, kila mmoja akionyesha umahiri wake. Wekundu wa Msimbazi hao wameweka kambi kwenye hoteli ya Royal Marang katika Mji wa Rustenburg, ikiwa ni umbali wa kilomita 120 kutoka jijini Johannesburg, wakitumia Uwanja wa Bafoken Sports Campus, kufanyia mazoezi. Utamu […]

Kutoka CR7 mpaka Maguire, inashtua kidogo

AYOUB HINJO MIAKA 33 iliyopita, Chuo Kikuu cha madawa nchini Marekani, Maryland, kilitoa tafiti yao kuhusu chanzo cha maradhi makubwa yanayowasumbua wanadamu. shinikizo la damu (presha) na Moyo. Katika tafiti hiyo, wataalamu wa Maryland walieleza kuwa, kwa asilimia 30 mwanadamu hujitengenezea mwenyewe maradhi hayo kupitia mawazo anayoyawaza. “Vitu tunavyoviwaza kila siku, ndivyo vitu vinavyotumaliza kila siku” Tunawaza nini? Kwanini? Na […]

Stars kusaka tiketi ya AFCON 2021 Oktoba

WINFRIDA MTOI KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho Soka Afrika (CAF), limefanya marekebisho ya michezo ya kufuzu michunao ya Kombe la Matiafa Afrika(AFCON 2021), itakayofanyika Cameroon. Marekebisho hayo yalifanyika katika kikao cha kamati hiyo kilichofanyika Jumatano wiki hii, hatua ya awali ikipangwa kuanza Oktoba7-15, 2019. Michezo nyingine itachezwa kati ya Novemba 11-19, mwaka huu, huku ikirudiana Agosti 31 na Septemba 8, […]