Category: Burudani

Hongera Harmonize kumrejesha Q Chilla

NA CHRISTOPHER MSEKENA MTINDO wa staa wa Bongo Fleva kutoka WCB,  Rajab Kahali ‘Harmonize’, kurudisha fadhila kwa wanamuziki wa zamani waliokuwa na mchango kwenye sanaa, umeendelea kushika kasi huku akipongezwa na watu mbalimbali wanaojua umuhimu wa wakongwe hao. Harmonize ambaye ni bosi wa Konde Gang, familia ya vijana wenye mawazo mchanganyiko ya kuweza kusaidia na jamii na vijana kutoka mtaani, […]

Shubira Stanton ndiye Miss Morogoro

NA JEREMIA ERNEST, MOROGORO MREMBO Shubira Stanton, ameibuka mshindi wa shindano la Miss Morogoro lililofanyika mwishoni mwa wiki mkoani humo akifuatiwa na Morine Kahayan a Veronica Royal. Akizungumza na Papaso la Burudani, mwandaaji wa Miss Morogoro, Farida Fujo, alisema anawashukuru wadau pamoja na wakazi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi katika shindano hilo. “Nawashukuru wakazi wa Morogoro na wadau wa […]

Silva M_A aendelea kupeta Marekani

MASSACHUSETTS, MAREKANI KUTOKA Massachusetts nchini Marekani, mwanamuziki wa kizazi kipya mwenye asili ya Kongo, Silva Matimano  ‘Silva M_A’, amemshukuru Mungu kwa kumpa mashabiki wanaounga mkono kazi zake kila anapotoa wimbo mpya.  Silva M_A, ambaye hivi karibuni aliachia wimbo ‘Come To Me’ aliomshirikisha DX Thunda, ameliambia Papaso la Burudani kuwa anajivunia kuiwakilisha Afrika Mashariki kwenye muziki nchini humo. “Sasa hivi nimetoa […]

RWANDA KWA WCB HUWAAMBII KITU

NA TIMA SIKILO, RWANDA UNAAMBIWA kama ambavyo staa wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ na wasanii wake wa WCB wanavyokubalika Tanzania, hapa nchini Rwanda pia hali iko hivyo hivyo kwa nyimbo za wanamuziki hao kuchezwa katika mitaa mbalimbali. Imezoeleka mashabiki wa nchi fulani kupenda kusikiliza nyimbo za wasanii wao ila kwa upande wa Rwanda hali ni tofauti kwani Diamond […]

Conte aishangaa Inter Milan kuchelewesha dili la Lukaku

MILAN, Italia INTER Milan wamepata ubaridi, baada ya kuambiwa walipe pauni milioni 75 ili waweze kupata saini ya straika wa Manchester United, Romelu Lukaku. Suala hilo linaonekana kumchosha kocha wa Inter Milan, Antonio Conte ambaye alimfanya Lukaku chaguo la kwanza kusajiliwa ndani ya kikosi hicho cha mabingwa wa zamani wa Italia. Hivi sasa straika huyo yupo nchini Singapore na kikosi […]

Ngassa anukia unahodha Yanga

MICHAEL MAURUS BAADA ya Ibrahim Ajib kuondoka Yanga, kitambaa cha unahodha ndani ya timu hiyo kwa sasa kipo wazi kwa wachezaji watatu, miongoni mwao, akiwa ni winga machachari, Mrisho Ngassa. Ajib aliyetimkia Simba baada ya mkataba wake Jangwani kumalizika, alipewa cheo hicho kutoka kwa Kelvin Yondani, huku msaidizi wake, akiwa ni Juma Abdul. Lakini wakati nafasi kubwa ya unahodha ikionekana […]

Kaseja ajifua kivyake kumkabili Manula Stars

ZAINAB IDDY KIPA Juma Kaseja ameendelea kujifua kivyake, licha ya kocha wa timu yake ya KMC,  Jackson Mayanja,  kuwapa mapumziko ya siku tatu, baada ya kurejea nchini wakitokea Kigali, Rwanda kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu Kombe la Kagame. KMC iliyoshiriki kwa mara ya kwanza michuano ya Kagame ilishindwa kutinga robo fainali kutokana na kufanya vibaya […]

Uwoya, Barnaba kuipamba Miss Moro

MICHAEL MAURUS, MOROGORO MSANII mahiri wa filamu, Irene Uwoya na mkali wa Bongo Fleva, Barnaba, wanatarajiwa kupamba kinyang’anyiro cha Miss Morogoro 2019, kwenye ukumbi wa Morogoro Hoteli, mjini hapa leo, huku kukiwa na shoo kali kutoka kwa mkali wa muziki wa dansi, Christian Bella. Kwa mujibu wa mratibu wa shindano hilo, Farida Kulususu, jumla ya warembo 12 watapanda jukwaani kuwania […]

Dkt. Msolla aja na mkakati kabambe

MICHAEL MAURUS, MOROGORO MWENYEKITI wa Yanga, Dkt. Mshindo Msolla, amepanga kukutana na mchezaji mmoja mmoja ili kuwaweka sawa kabla ya kuanza kwa msimu ujao, wakikabiliwa na michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika. Akizungumza na BINGWA jana alipotembelea mazoezi ya timu hiyo ya asubuhi yaliyoambatana na mechi ya kirafiki dhidi ya Moro Kids, kwenye Uwanja wa […]