CASILLAS: NEYMAR KWA RONALDO? MADRID VIPI NYIE

Lisbon, ureno


 

KIPA wa FC Porto, Iker Casillas, ameiambia klabu yake ya zamani ya Real Madrid kuwa, itakuwa biashara kichaa kuwapa PSG huduma ya Cristiano Ronaldo ili wampate Neymar.

Tayari kuna shaka juu ya hatima ya Ronaldo pale Bernabeu, hasa baada ya kutotokea wakati timu hiyo ikitambulisha uzi wake mpya wa msimu ujao.

Pia, ni muda mrefu sasa Madrid wamekuwa wakimmezea mate Neymar, ambaye ameelezwa kutofurahia maisha yake mapya katika klabu ya PSG.

“Cristiano ni mchezaji bora zaidi niliyewahi kufanya naye kazi. Watu wanazungumza upuuzi (kuwa ataondoka). Anafurahia maisha ya Madrid. Cristiano anaweza kufananishwa na (Alfredo) Di Stefano (lejendari wa Madrid).

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*