googleAds

Casillas kusuka au kunyoa

LISBON, Ureno

KIPA wa zamani wa Real Madrid, Iker Casillas ameambiwa na madaktari, kutoa maamuzi endapo ataendelea kucheza soka au kutundika daruga.

Kwasasa Casillas mwenye umri wa miaka 38, anasumbuliwa na matatizo ya moyo, iliyompelekea kudondoka kutokana na mshtuko mwaka jana, akiwa mazoezini na wachezaji wenzake.

Hata hivyo ndugu wa karibu wa mkongwe huyo anayekipiga Porto ya Ureno, amesisitiza Casillas anaendelea vizuri lakini madaktari wamejawa na hofu juu ya afya yake.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*