googleAds

Bunge SC kwenda Uganda Jumapili

 NA RAMADHAN HASSAN,DODOMA

TIMU ya  Bunge  imepanga kuondoka Jumapili kwenda jijini Kampala Uganda kushiriki michuano ya mabunge ya Afrika Mashariki.

Akizungumza na BINGWA jana jijini hapa, Kocha wa timu ya Bunge, Venance Mwamoto,  alisema michuano hiyo imepangwa kuanza Jumatatu ijayo.

Mwamoto alisema wanaendelea kufanya mazoezi makali kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani hapa kujiandaa na michuano hiyo.

Alisema katika michuano hiyo watawakosa wachezaji muhimu akiwamo, Mwigulu Nchemba na Ridhiwani Kikwete ambao wana majeraha.

“Kesho (leo) tunacheza mchezo wa kirafiki na timu ya Waandishi wa Habari katika Uwanja wa Jamhuri, tupo vizuri na tuna uhakika wa kufanya vizuri katika mashindano hayo,”alisema Mwamoto.

Timu nyingine zinazojipanga kwenda Uganda kushiriki michuano hiyo ni netiboli, riadha, kuvuta kamba  ambazo zinaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Jamhuri.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*