Bosi waamuzi haja na hili

NA ZAINAB IDDY

ALIYEWAHI kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Salum Chama, amesema kuwa anatarajia kuona marefa wakifanya kazi kwa ufanisi zaidi ya awali kutokana na wengi wao kutumia muda wa mapumziko kujifunza mengi yanayohusu kazi hiyo.

Akizungumza na BINGWA jana, Chama alisema kuwa kwa muda wa miezi zaidi ya miwili ambayo ligi imesimama, ana uhakika waamuzi wanaopenda kazi yao watakuwa wameutumia kurejea sheria na kanuni mbalimbali za mchezo wa soka.

“Ni zaidi ya miezi miwili sasa tangu ligi iliposimama kutokana na janga la corona, ulikuwa muda mzuri kwa waamuzi kuzirejea kanuni na sheria zinazotumika katika soka.

“Nawaamini waamuzi wote, hivyo baada ya ligi kurejea, watafanya kazi zao kwa ufanisi kwa kuzingatia sheria za soka, lakini pia kila timu iweze kutoka uwanjani huku kukiwa hakuna malalamiko kama ilivyokuwa awali,” alisema.

Chama aliongeza kuwa soka ni burudani ambayo kila shabiki atahitaji kuona anapata kitu kizuri na waamuzi ni sehemu ya kufanikisha hilo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*