googleAds

Bosi mpya Simba akumnjulia makucha Aussems

NA MWANDISHI WETU


MTENDAJI Mkuu wa klabu ya Simba, Senzo Mazingiza amelichimba mkwara benchi la Ufundi la timu hiyo chini ya Kocha Patrick Aussems kwa kitendo cha kuwapa mapumziko ya siku mbili wachezaji mara baada ya kurudi kutoka Kanda ya Ziwa.


Taarifa za uhakika kutoka ndani ya uongozi wa Simba, zimelieleza DIMBA Jumatano,Mazingiza amekasirisha na uamuzi wa benchi la ufundi kuwapumzisha wachezaji huku yeye akiwa hajahusishwa kama bosi wa timu hiyo.


“Mtendaji wetu mkali sana hataki masihara hata kidogo, amemwambia kocha wetu wazi wazi kwamba ilikuwaje akawapumzisha wachezaji bila kumpa taarifa kitendo ambacho amekichukulia ni utovu wa nidhamu kwake, hivyo amemjia juu Aussems kwa kumuonya,”alisema mtoa taarifa.


Chanzo hicho kimesema Mtendaji huyo ameapa kutokumbatia utovu wa nidhamu wowote utakaoonyeshwa na mchezaji au mtu yoyote katika benchi la ufundi.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*