BOCCO AFUNGIWA MECHI 3

NA ZAITUNI KIBWANA


 

KAMATI ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi imemfungia kucheza mechi tatu nahodha wa timu ya Simba, John Bocco, pamoja na kumtoza faini ya Sh 500,000.

Uamuzi huo ulitolewa jana kutokana na adhabu ya straika huyo kuonyeshwa kadi nyekundu katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mwadui FC kwa kosa la kumpiga ngumi kichwani mchezaji, Revocatus Richard.

Katika mchezo huo ambao Simba walishinda mabao 3-1 katika Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga, Bocco alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 79 na mwamuzi, Alfred Vitalis kutoka mkoani Kilimanjaro baada ya kumpiga mchezaji huyo wa Mwadui.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB), Boniface Wambura, alisema adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 38(9) ya Ligi Kuu inahusiana na udhibiti wa wachezaji.

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la BINGWA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*