googleAds

Bocco aanza mdogomdogo

NA WINFRIDA MTOI

STRAIKA na nahodha wa Simba, John Bocco, ameanza mazoezi mepesi na kikosi hicho kinachojifua katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.

Bocco alipata majeraha katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC uliyochezwa Agosti 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Tangu hapo, Bocco amekuwa chini ya uangalizi wa madaktari na alikuwa haonekani hata mazoezini, lakini juzi alianza kuonekana rasmi.

Katika mazoezi ya jana, Bocco alianza kwa kufanyiwa matibabu na mtaalamu wa tiba ya viungo wa klabu hiyo, Mjerumani, Paulo Gomez Dardenne, kisha kutembea naye taratibu.

Baada ya zoezi hilo la dakika kadhaa, alimkabidhi kwa kocha wa viungo, Adel Zrane, ambaye aliendelea kumfanyisha mazoezi mepesi ya viungo.

Majeruhi wengine wa Simba ambao hali zao zimetengemaa na kuungana na wenzao kufanya mazoezi ya pamoja ni beki wa kati, Pascal Wawa na straika raia wa Brazil, Wilker Henrique Da Silva.

Bocco hakuonekana uwanjani katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya UD Songo na ule wa Ligi Kuu Tanzania Bara na JKT Tanzania.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*