googleAds

Bilo awakomalia akina Tegete

WINFRIDA MTOI

KOCHA wa Alliance , Athuman Bilali ‘Bilo’, amesema anaendelea kuifua safu ya ushambuliaji wa timu hiyo, ili iweze kufunga mabao mengi msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaoanza Agosti 23, mwaka huu.

Miongoni mwa washambuliaji waliosajiliwa na timu hiyo ni Jerryson Tegete na Six Mwasekage ambao katika mechi mbili za kirafiki walizocheza wamefunga mabao matatu.

Akizungumza na BINGWA jana, Bilo alisema hana wasiwasi na safu yake ya ulinzi, kwani tayari imekaa sawa, anachofundisha kwa sasa ni eneo la kiungo na ushambuliaji.

Bilo alisema atamaliza programu yake ya mazoezi baada ya kuona eneo hilo limekaa vizuri.

Alisema katika mechi za kirafiki walizocheza, walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tanzania Prisons na juzi alitoka kutoka sare ya bao 1-1 na Pamba  na kukuona bado anahitaji kuongeza nguvu katika ushambuliaji.

“Mabao tuliyofunga kwa mechi zote, Tegete amefunga moja na Mwasekage mawili, huku washambuliaji wengine wakishindwa kufunga kabisa, hali inayonifanya nilitazame eneo hili zaidi kwa sababu mpira ni mabao,” alisema Bilo.

Alisema katika kurekebisha eneo hilo, anatarajia kucheza mechi na Rhino Rangers, Singida United na Tusker FC ya Kenya ndani ya wiki hii.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*