googleAds

BIEBER AKATAA UBAGUZI WA RANGI

LOS ANGELES, Marekani

LICHA ya vituko vyake, mwanamuziki wa pop, Justin Bierber, ameonesha kutounga mkono ubaguzi wa rangi unaoendelea nchini Marekani dhidi ya raia wenye asili ya Afrika.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23, amesema atafanya anachokiweza kukomesha tabia hiyo ili kuhakikisha usawa unapatikana.

Bierber alitumia akaunti yake ya mtandao wa Instagram kuunga mkono  kampeni ya kupinga matukio ya ubaguzi inayoitwa Black Lives Matter Movement.

Mkali huyo wa ngoma ‘Sorry’ aliandika: “Mimi ni mtu mweupe kutoka Canada na sitaki kujua maana ya kuwa Mmarekani mwenye asili ya Afrika.

“Lakini ninachokijua ni kwamba niko tayari kusimama na kutumia sauti yangu kukemea ubaguzi,” aliandika Bierber.

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*