googleAds

Bi Mwenda afunguka kuchezea kichapo

NA JEREMIA ERNEST

MWIGIZAJI mkongwe nchini, Fatma Makongoro ‘Bi Mwenda’, amesema mara kadhaa amewahi kuchezea kichapo kutoka kwa mashabiki zake ambao huwa wanadhani ni mshirikina kama anavyoigiza katika filamu na tamthiliya mbalimbali.

Akizungumza na Papaso la Burudani jana, Bi Menda, anayefanya vizuri katika tamthiliya ya Huba, alisema amefanikiwa kuvaa uhusika wa ushirikina katika tasnia ya filamu mpaka baadhi ya mashabiki wanadhani ni mchawi kweli.

“Napitia changamoto nyingi kutokana na uhusika wa uchawi, wengine wanadiriki kunipiga ila sijawahi kuwarudishia nafurahi kwa kuwa ujumbe unafika katika jamii, hata familia yangu pia huwa inanitilia mashaka ila sijawahi kukata tamaa kwa sababu siyo kweli na ile ni kazi tu,” alisema Bi Mwenda.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*