Berbatov ataka mashabiki wabaguzi wafungiwe maisha

SOFIA, Bulgaria 

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Tottenham, Dimitar Berbatov, amewaponda mashabiki wa Bulgaria waliyoonyesha vitendo vya kibaguzi na kuitaka Shirikisho la Soka nchini humo (BFF) kuwafungia maisha kujihusisha na masuala ya soka.

Kitendo cha mashabiki hao kuwaita nyani wachezaji weusi kutoka England, kimemkera na amekilaani.

Tukio hilo limetokea wakati England ilipomenyana na Bulgaria katika mechi ya kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya (Euro 2020) hivi karibuni.

“Lazima kutakuwa na watu waliochochea, hawa watu hawastahili kabisa kuwepo kwenye soka, maoni yangu, wafungiwe maisha wasijihusishe na soka, jambo la aibu sana na kufedhesha,” alisema Berbatov. 

Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Gianni Infantino, ameingilia kati suala hili la wachezaji weusi kubaguliwa na kutaka hatua kali zichukuliwe.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*