BENDTNER ‘MVUNJA TAYA’ AOMBA MSAMAHA

COPENHAGEN, Denmark


 

SIKU chache baada ya kutiwa nguvuni kwa madai ya kumvunja taya dereva taxi, straika wa zamani wa Arsenal, Nicklas Bendtner, ameibuka na kuomba msamaha.

Straika huyo ambaye kwa sasa anaitumikia klabu ya Rosenborg ya Denmark, alitajwa na dereva huyo kwamba alihusika katika tukio lililosababisha avunjwe taya wikiendi iliyopita jijini Copenhagen na vyanzo vya habari viliripoti kukamatwa kwake.

Ripoti iliyotolewa na jarida la Denmark, Ekstra Bladet, lilieleza kuwa Bendtner alionekana kwenye tukio hilo saa kadhaa baada ya kumaliza ‘kula bata’ na mchumba wake, Philine Roepstorff, kwenye klabu ya usiku ya Lusso.

“Najutia tukio hilo ambalo mmelisikia likitangazwa na vyombo vya habari ndani ya siku chache zilizopita kuwa nilihusika kwenye fujo zilizotokea Jumapili. Sikudhani kama ingesambaa namna hiyo, niiombe klabu na mashabiki wangu msamaha.

“Kusema kweli najutia kwanini sikujizuia nisiwepo katika matukio kama hayo.”


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*