googleAds

Beki KMC ajipa matumaini kwa AS Kigali

GLORY MLAY

BEKI wa timu ya KMC, Abdallah Mfuko, amesema  anamatumaini ya kushinda katika mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya AS Kigali utakaochezwa  kati ya Agosti 23, 24  na 25 mwaka huu,  kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa wiki iliyopita, Kigali, Rwanda,timu hizo zilitoka sare ya kutofungana, hiyo KMC wanahitaji ushindi nyumbani ili waweze kusonga mbele.

Akizungumza na BINGWA jana, Mfuko alisema kama watapambana vilivyo katika mchezo huo wanaweza  kushinda na kutinga hatua itakayofuata.

Mfuko alisema anaamini kocha wao, Jackson Mayanja atafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika mchezo wa awali kabla ya kukutana na AS Kigali.

 “Malengo yetu tuliyotarajia katika mchezo wa kwanza  hayakutimia,  lakini hatupaswi kuvunjia moyo, bado tuna nafasi ya kusonga mbele kikubwa ni kupambana   kwa kuwa kila kitu kinawezekana.

“Tupo nyumbani na kila mchezaji atatakiwa kujituma ili tuwafunge hawa wapinzani wetu na tusonge hatua inayofuata,” alisema Mfuko.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*