Barca: Valverde ataendelea kuwa hapa

CATALUNYA, Hispania

TAARIFA iliyotolewa na Barcelona kupitia rais wao, Josep Bartomeu, imedai kuwa hawana mpango wa kuachana na kocha wao, Ernesto Valverde.

Si tu Valverde atakuwa kocha wa Barca msimu ujao, pia ni kocha wa mipango ya muda mrefu ya klabu hiyo, kwa mujibu wa Rais Bartomeu.

Valverde alikuwa akiinoa Athletic Bilbao kabla ya kuitwa Camp Nou msimu wa 2017-18 ili kwenda kuchukua kibarua cha Luis Enrique.

Tetesi za kutimuliwa kwake zilikolezwa na kitendo cha timu hiyo kung’olewa na Liverpool katika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, licha ya ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*