BALOTELLI KUPEWA UNAHODHA ITALIA

MILAN, Italia


KOCHA mpya wa timu ya Taifa ya Italia, Roberto Mancini, amesema straika wake mtukutu, Mario Balotelli, anaweza kupewa kitambaa cha unahodha wa kikosi hicho.

Baada ya kuwa nje ya timu hiyo kwa miaka minne, Balotelli alianza kuichezea Italia hivi karibuni akiitwa na Mancini.

Mancini amewahi kutaka kuzichapa na Balotelli wakati akiwa naye Manchester City, lakini amekuwa akikiri kuwa ni mmoja kati ya wachezaji anaowakubali.

“Katika timu ya taifa, mara nyingi kitambaa cha unahodha huenda kwa mchezaji aliyecheza mechi nyingi.

“Kama Balotelli atakuwa kikosi cha kwanza na akawa amecheza mechi nyingi, anaweza kuwa nahodha,” alisema Mancini.

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*