Bale agoma kutimka Madrid

MADRID, Hispania

NYOTA wa Real Madrid, Gareth Bale, hana mpango wa kuondoka klabuni hapo kama inavyoelezwa na vyombo vya habari barani Ulaya.

Hiyo ni kwa mujibu wa wakala wake, Jonathan Barnett, aliyesema mchezaji huyo anataka kulimalizia soka lake Santiago Bernabeu.

Kauli ya wakala huyo inakuja baada ya kuwapo kwa tetesi kuwa Bale na kocha aliyerejea, Zinedine Zidane, ni ‘chui na paka’, hivyo anasaka mlango wa kutokea.

Akikanusha taarifa hizo katika mahojiano yake na kituo cha televisheni cha BBC Sport, Barnett alisema: “(Bale) anataka kuzeekea Real Madrid na kama kutakuwa na kipingamizi, basi tutakaa tena mezani.”


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*