googleAds

Bahati Simwiche kuzindua ‘Viwango’ Mbeya

NA SISCA MACHABA (TUDARCo)

MWIMBAJI mahiri wa Injili nchini, Bahati Simwiche, amewaomba wakazi wa Jiji la Mbeya kujiandaa kupokea uzinduzi wa albamu yake mpya ‘Viwango’, utakaofanyika Jumapili wiki hii katika Kanisa la Redeemed Church Kabwe kwa Mtume Mwakajinga.

Akizungumza na Papaso la Burudani jana, Simwiche alisema albamu hiyo ina nyimbo zenye mguso wa kipekee.

“Nitasindikizwa na waimbaji wengi kama Maria Msalilwa, Janeth Mwani, Beatrice Swai, Jesca Gazuko, Asia Masimbani, Mary Edson, Happy Sanga, Enock Mwambepo, Sospeter Joel, Mwasaga, Yoabu Nzala na Angel Shadrack,

“Wengine ni Kefa Kyalo, Daniel Isingo, Rachel Daniel, Ikupa Mwambeja, Emma Mbasha, Tumaini Mbembela, Lenny, Mnene Makweta, Martha Antony, Fabian Modern, Emmy Benny, Mtume Mwansasu, Samadani na wengineo wengi,” alisema Simwiche.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*