BABU TALE AFIKISHA 50% KUWARUDISHA DIAMOND, ZARI

NA CHRISTOPHER MSEKENA


 

 SIKU chache baada ya staa wa Bongo Fleva, Nasib Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuachia wimbo wa Iyena ambao umegonga vichwa vya habari za burudani Afrika Mashariki, Meneja Babu Tale, anakaribia kumaliza tofauti za Zari The Boss Lady na msanii huyo.

Babu Tale ambaye mwishoni mwa wiki alisafiri kwenda Pretoria, Afrika Kusini nyumbani anakoishi Zari na wanawe Tiffah na Nillan, jana aliwafahamisha mashabiki wanaofuatilia sakata hilo kupitia ukurasa wake wa picha kuwa tayari amefikisha asilimia 50 kuwarudisha mapenzini Diamond Platnumz na mrembo huyo wa Kiganda.

“Karibu asilimia 50 nimemaliza, asante mama Tee (Zari),” alisema Babu Tale.

Wakati hayo yakiendelea, usiku wa kuamkia jana Diamond aliungana na mastaa wengine Afrika kama vile Vanessa, Akothee kufanya maonyesho ya aina yake katika tamasha la One Africa huko Uingereza, huku mvutano mkali ukiendelea kati ya familia, wasanii wa WCB na mashabiki kuhusu mrembo wa kuolewa na staa huyo kati ya Zari, Wema Sepetu na Hamisa Mobetto.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*