googleAds

BABA YAKE AUBAMEYANG KUINOA GABON

LIBREVILLE, Gabon

BABA mzazi wa straika Pierre-Emerick Aubameyang, ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Gabon, taarifa ya Shirikisho la Soka la nchini humu (Fegafoot) imesema.

Pierre Francois Aubameyang, ambaye pia aliwahi kuwa mchezaji wa timu hiyo, amepata shavu hilo, sambamba na mkongwe mwingine, Daniel Cousin.

Kutua kwa wawili hao kumetokana na pengo lililoachwa wazi na kocha wa Kihispania, Jose Antonio Camacho, aliyeachia ngazi baada ya kumalizika kwa mkataba wake.

Kibarua cha kwanza cha mzee Aubameyang (53) kitakuwa ni kuihakikishia Gabon tiketi ya kwenda kucheza fainali za Afcon 2019 ambazo zitafanyika Cameroon.

Mechi ya kwanza ya ushindani ni ile ya mwezi ujao, ambapo kikosi chake kitamenyana mara mbili (nyumbani na ugenini) na Sudan Kusini.

Kwa upande wake, Cousin, mwenye umri wa miaka 41, aliwahi kucheza Ligi Kuu ya England akiwa na Hull City, kabla ya baadaye kutamba Scotland alikokuwa akiichezea Glasgow Rangers.

Pia, alicheza Ufaransa na Ugiriki na kwa kipindi chote alichokuwa na Gabon, aliifungia mabao 13 katika mechi 53, ikikumbukwa kuwa alikuwa nayo katika fainali za Afcon za mwaka 2000, 2010 na 2012.

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*