googleAds

AZAM YAANZA VITA RASMI

NA TIMA SIKILO

LICHA ya kocha wa Azam FC, Etienne Ndayiragije, kukabiliwa na majukumu mengine ya kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, amemuachia programu za maana kocha msaidizi, Idd Nassor ‘Cheche’.

Azam FC inatarajia kuvaana na Simba Oktoba 23 mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, ambapo vikosi hivyo vitakuwa vinakutana kwa mara ya pili baada ya mwezi mmoja.

Ndayiragije alialiambia DIMBA Jumatano kuwa kwa sasa yuko bize na Taifa Stars lakini hakuna kitakachoharibika akitambua mchezo unaofuata ni mgumu.

“Kila timu inajiandaa, hivyo atakayejiandaa vya kutosha ndiyo atakaye shinda, siwezi kujipa uhakika wa ushindi kwa asilimia ngapi lakini tutajitahidi kufanya mazoezi ya kutosha,” alisema.

Mara ya mwisho Simba na Azam FC kukutana ilikuwa katika mchezo wa Ngao ya Jamii, ambapo Wekundu wa Msimbazi waliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 3-1.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*