Author: Bingwa

Kocha wa Serengeti Boys piga kazi yako

NA JONATHAN TITO KITENDO cha Serengeti Boys kufungwa 5-4 na Nigeria katika mchezo wa kwanza wa Kombe la Mataifa ya Afrika ya vijana chini ya umri wa miaka 17, kimehuzunisha Watanzania wengi. Mbaya zaidi ni kwa jinsi timu hiyo ya vijana ambayo iliandaliwa kwa takribani miaka minne na kuonekana kushindwa kucheza kwa kiwango kile kilichotarajiwa na wengi. Kikosi hicho kimepambana […]

Kenny Guitar Mkali wa gitaa aliyeupaisha wimbo ‘You Are The Best’ wa Ommy Dimpoz

NA CHRISTOPHER MSEKENA MIONGONI mwa wimbo unaokonga mioyo ya watu kwa sasa hapa Bongo ni You Are The Best wa mwimbaji, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, iliyonogeshwa kwa gitaa asili ya Hispania na kufanya wimbo huo uwe burudani kwa yeyote anayesikiliza. BINGWA lilikutana na mpiga gitaa la solo, Kennedy Masanja ‘Kenny Guitar’, ambaye ndiye alipiga chombo hicho kwenye wimbo huo ambao […]

Kongamano la filamu liwatoe gizani waigizaji

NA CHRISTOPHER MSEKENA MAPEMA jana jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa JKT, Mwenge, lilifanyika kongamano kubwa la wasanii wa filamu likiwa limepewa nguvu na Bodi ya Filamu Tanzania na Chama cha Waigizaji. Lengo kuu la kongamano hilo ambalo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, lilikuwa ni kuwajengea uwezo wasanii katika nyanja […]

Minziro: Nina kibarua kigumu Singida United

WINFRIDA MTOI KOCHA wa Singida United, Fred Minziro, amekiri ana kibarua kigumu cha kuirejesha timu hiyo kwenye chati na kuhakikisha inakaa nafasi za juu katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Singida United inashika nafasi ya 10 katika msimamo wa ligi hiyo, kutokana na pointi 40, baada ya kucheza michezo 33 na kushinda 10, sare 10 na kupoteza 11. Akizungumza […]

Kwesi Appiah ‘ang’atwa’ sikio Afcon 2019

ACCRA, Ghana  NYOTA wa zamani wa timu ya Taifa ya Ghana ‘Black Star’, Ibrahim Sunday, amemg’ata sikio kocha wa sasa, James Kwesi Appiah, kuwa makini katika uteuzi wa wachezaji ambao atakwenda nao katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, Afcon, 2019 zitakazofanyika miezi michache ijayo nchini Misri. Katika fainali hizo zitakazoanza kutimua vumbi kuanzia Juni hadi Julai mwaka huu, […]

Kocha Serengeti Boys kupangua kikosi

TIMA SIKILO KOCHA wa timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’, Oscar Milambo, amesema anatarajia kupangua kikosi ili kuepuka kichapo katika mchezo utakaofuata wa kuwania ubingwa wa michuano ya Afrika kwa vijana. Serengeti Boys wanatarajiwa kucheza na Uganda katika mchezo wa Kundi A, utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, baada ya […]

Sterling amwagiwa sifa kibao

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, amepewa sifa kibao na mchambuzi wa kituo cha Sky Sports, Ian Wright, baada ya mchezaji huyo kufunga mabao mawili dhidi ya Crystal Palace. Timu hiyo inayonolewa na Pep Guardiola, walishinda mabao 3-1 huku Gabriel Jesus akifunga bao jingine kati ya hayo, lakini Sterling alionekana kumfurahisha zaidi mchambuzi huyo. “Kila siku anakuwa mpya […]

Yanga yatua Moro na hesabu kali

HUSSEIN OMAR NA ZAITUNI KIBWANA KIKOSI cha Yanga tayari kimetua mjini Morogoro kikiwa na hesabu kali za kuhakikisha wanashinda mchezo wao wa kesho dhidi ya Mtibwa Sugar, utakaopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro. Yanga ndio vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kukusanya pointi 74, wakicheza mechi 31, ambapo wameshinda 23, sare tano na kufungwa tatu. Akizungumza na BINGWA […]