Author: Bingwa

Zahera kuivamia Mbeya City usiku wa manane

WINFRIDA MTOI NA TIMA SIKILO KOCHA Mwinyi Zahera ameshindwa kuungana mapema na wachezaji wake wa Yanga ambao wanatarajiwa kuondoka leo asubuhi kwenda Mbeya kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Vinara hao wa Ligi Kuu keshokutwa watacheza dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine, huku kocha wao akishindwa kutua jana kutokana na ndege aliyotakiwa kusafiri nayo […]

Cardi B kweli kivuruge

LOS ANGELES, Marekani RAPA anayefanya vizuri kwa upande wa wanawake, Cardi B, juzi alionekana akiwa na aliyekuwa mume wake, Offset, Puerto Rico, Kusini Mashariki mwa Miami, Marekani. Ishu ni kwamba, alipoulizwa sababu ya kukutana na Offset wakati alishaachana na jamaa huyo, ndipo alipowaacha vinywa wazi mashabiki wake. Alichokisema Cardi B kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram ni […]

Rihanna na yule Mwarabu wamerudiana au?

LOS ANGELES, Marekani MWANZONI mwa Novemba mwaka huu ilifichuka kuwa wameshaachana na kila mtu amechukua ‘50’ zake. Hata hivyo, hivi karibuni Rihanna na bilionea mwenye jina kubwa huko Saudi Arabia, Hassan Jameel, wameonekana wakiwa pamoja hivyo kuibua minong’ono kuwa huenda wameyamaliza. Kamera za waandishi wa habari za burudani ziliwanasa wakiwa nje ya mgahawa mmoja mjini Malibu, Marekani. Wakati ikifahamika kuwa […]

Yanga wampigia magoti Zahera

HUSSEIN OMAR WACHEZAJI wa zamani wa Yanga wakiongozwa na Sunday Manara, wamepanga kukutana na kocha mkuu wa timu hiyo, Mwinyi Zahera, kwa ajili ya kumwomba msamaha kutokana na madudu ya usajili yaliyofanywa na viongozi wa klabu hiyo. Akizungumza na BINGWA jana, Mwenyekiti wa Umoja wa Wachezaji wa zamani wa Yanga, Ramadhan Kampira, alisema wamefedheheshwa na kitendo cha udanganyifu kilichofanywa na […]

Aussems: Tumezima jeuri ya Nkana FC

MWAMVITA MTANDA KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, ametamba kuwa wamezima jeuri ya Nkana FC ambao walikuwa wanakidharau kikosi chao kutokana na historia ya muda mrefu wakiamini itajirudia, lakini wamegonga mwamba mikononi mwake. Simba imefanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuichapa Nkana FC mabao 3-1 katika mechi ya marudiano iliyochezwa juzi kwenye Uwanja wa […]

Chama awatangazia vita vigogo Afrika

*Aliyemleta asema atashusha vifaa vingine WINFRIDA MTOI KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Cletus Chama, amezitangazia vita klabu za Afrika zilizotinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Nyota huyo wa Zambia, Chama, juzi alifunga bao muhimu dhidi ya Nkana FC lililoivusha timu yake ya Simba hatua ya makundi na kupiga mkwara huo mzito. Katika mchezo huo wa marudiano, Simba walikuwa […]

Samatta ajipa zawadi ya ‘birthday’ yake

MWANDISHI WETU MSHAMBULIAJI wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Samatta anayekipiga KRC Genk, juzi alijipa zawadi yake ya siku ya kuzaliwa kwa kupachika mabao mawili dhidi ya KAS Eupen. Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Ubelgiji ‘Jupiler Pro League’, ulichezwa juzi Jumamosi, Desemba 23, tarehe ambayo nahodha huyo wa Taifa Stars alizaliwa. KRC Genk walishinda mchezo huo […]

Kocha adai Lyon hawashuki daraja

NA TIMA SIKILO KOCHA wa African Lyon, Adam Kipatacho, amesema hawakati tamaa na watapambana hadi mwisho kuhakikisha wanabaki Ligi Kuu Tanzania Bara. Kikosi hicho cha Lyon kilichapwa bao 1-0 kwenye mchezo wao wa mwisho wa Ligi Kuu na kuifanya ishike nafasi ya 18 katika msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi 12 kati ya michezo 17 waliyocheza. Akizungumza na BINGWA […]