Author: Bingwa

CAMPBELL ATAJA WA KUMRITHI WENGER

LONDON, England     NYOTA  wa zamani Arsenal, Sol Campbell, amewataja mastaa wenzake wa zamani, Patrick Vieira na Dennis Bergkamp, kuwa watu mbadala wa kukinoa kikosi cha kwanza cha Gunners wakati kocha wa sasa, Arsene Wenger, atakapoondoka. Wenger alitangaza kuitema Arsenal mwishoni mwa wiki iliyopita ifikapo mwishoni mwa msimu huu, ikiwa ni baada ya kuitumikia kwa muda wa miaka 22. […]

KIGOGO AS ROMA AJIPA MATUMAINI

ROMA, Italia   MKURUGENZI wa Michezo wa AS Roma, Ramón Rodríguez, maarufu kama Monchi, amesema kwamba, bado ana matumaini watasonga mbele hatua ya fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, licha ya kufungwa na Liverpool. Kigogo huyo alisema jana kuwa, matumaini hayo ni kutokana na kuwa na faida ya mabao mawili waliyoyapata dakika za mwisho za mchezo huo uliopigwa […]

JARIDA LAMUOMBA RADHI INIESTA

PARIS, Ufaransa   JARIDA la Michezo nchini Ufaransa limemuomba radhi mkongwe wa Barcelona, Andres Iniesta, kwa kushindwa kumpa tuzo ya mchezaji bora wa dunia, Ballon d’Or. Mhariri wa jarida hilo, Pascal Ferre, aliandika juzi katika maoni yake kumuomba radhi staa huyo na huku akimpongeza kwa kazi nzuri anayoifanya na huku akiacha mlango wazi kwa mwaka huu apewe nafasi hiyo kama […]

KLOPP AKIRI ANGEUMBUKA KWA KUMPUMZISHA MO SALAH

LONDON, England   KOCHA Jurgen Klopp amekiri akisema kuwa, angetwishwa lawama kwa uamuzi wake wa kumpumzisha staa wake, Mohamed Salah, baada ya straika hiyo kuwafanyia balaa waajiri wake wa zamani, AS Roma, katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Katika mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Anfield, Salah ndiye aliyetupia mabao mawili kipindi cha kwanza […]

YANGA: SIMBA HAWATAAMINI J’PILI

NA ZAITUNI KIBWANA     KOCHA Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, amesema wengi hawataamini kitakachotokea keshokutwa Jumapili, kwani wamepanga kushangaza mashabiki wanaowabeza kuelekea mchezo huo. Yanga, wenye pointi 48, watavaana na watani zao, Simba, Jumapili, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wameweka kambi […]

UKWELI MIL 600/- ZA YANGA

*CAF yataja siku zitakazotolewa, yasema Yanga wakituliza akili, kuongezwa midola ya kumwaga NA MICHAEL MAURUS MARA baada ya Yanga kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, kwa sasa mashabiki wao wamekuwa wakitambia kitita watakachopokea kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kutokana na mafanikio yao hayo. Wapo waliofika mbali kwa kuzipangia matumizi fedha hizo, wengi wakiamini zitalipa madeni ya […]

MAKOCHA 10 WANAOVUTA MKWANJA MREFU

MOSCOW, Urusi | KIU ya mashabiki wa soka ulimwenguni kote inasubiri kushuhudia fainali za Kombe la Dunia zinazotarajiwa kufanyika nchini Urusi, mwaka huu. Jumla ya mataifa 32 kutoka sehemu mbalimbali duniani yatakuwa yakionyeshana kazi katika ardhi ya Urusi, ambao wameweka historia ya kuandaa michuano hiyo kwa mara ya kwanza. Miongoni mwa watu wanaotarajiwa kuwa na presha kubwa ni makocha wa […]