Author: Bingwa

LWANDAMINA AFURAHIA KUREJEA ZESCO UTD

NA HUSSEIN OMAR | BAADA ya aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina, kurejea kwenye klabu yake ya zamani Zesco United na kutambulishwa jana, amesema amefurahia tena kuifundisha timu hiyo, baada ya mkataba wake na Yanga kumalizika. Kocha huyo ambaye ameiongoza Zesco kucheza mechi za mashindano ya kimataifa katika Ligi ya Mabingwa Afrika, mara 18, alitambulishwa rasmi jana na uongozi […]

ARSENAL ‘KUWAACHIA MANYOYA’ ATLETICO LEO?

LONDON, England   NI kufa au kupona dhidi ya Atletico Madrid. Arsenal leo wanahitaji ushindi au kama itashindikana, basi wapate sare ya kuanzia mabao 2-2. Mchezo mwingine wa nusu fainali ya Ligi ya Europa ni ule utakaozikutanisha Red Bull Salzburg itakayokuwa nyumbani dhidi ya Maresille iliyoshinda mabao 2-0 katika mtanange wa kwanza. Kwa upande wao, sare ya kutofungana haitawafaa Gunners […]

MASHABIKI LIVERPOOL ‘WATEKA’ BAA ITALIA

ROMA, Italia   KUELEKEA mchezo wao wa jana wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, idadi kubwa ya mashabiki wa Liverpool walionekana wakinywa pombe katika baa mbalimbali za jijini Roma. Mashabiki hao ni wale waliosafiri na timu kwa mchezo huo wa marudiano baada ya ule wa kwanza walioitandika Roma mabao 5-1 katika Uwanja wa Anfield. Gazeti la Sun liliripoti […]

AMESHINDIKANA RONALDO BWANA, SIKU HIZI HATA ASIPOFUNGA, ANAWEKA REKODI TU

  LONDON, England     UKIACHA mchezo wa juzi uliochezwa Santiago Bernabeu na kumalizika kwa sare ya mabao 2-2, Real Madrid na Bayern Munich walikutana katika Uwanja wa Allianz Arena, Ujerumani na wakali hao wa La Liga wakashinda mabao 2-1. Licha ya kutopasia nyavu katika mchezo huo wa usiku wa Jumatano ya wiki iliyopita, staa Cristiano Ronaldo aliweka rekodi kuwa […]

WEMA SEPETU ASHIRIKI UZINDUZI WA STAR TIMES KUONYESHA KOMBE LA DUNIA

  NA SALMA MPELI     MLIMBWENDE wa Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu pamoja na wasanii wengine mbalimbali, wameshiriki uzinduzi wa Star Times kuonyesha fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Juni 14 hadi Julai 15, mwaka huu nchini Urusi. Uzinduzi huo uliofanyika jana Ukumbi wa Terrace katika Hoteli ya Slipway jijini Dar es Salaam, ulihudhuriwa na wasanii hao wa Bongo […]

AJIB BADO ANA NAFASI KUWAFUTA MACHOZI YANGA

NA MICHAEL MAURUS   YANGA mwishoni mwa wiki hii inatarajiwa kuvaana na USM Ulger ya Algeria, katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, Wanajangwani hao wakiwa ugenini. Wakongwe hao wa soka nchini watashuka dimbani siku hiyo wakitoka kupoteza mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya watani wao wa jadi, Simba, walipopigwa bao 1-0 […]

UNAJUA BOCCO NI MWANAMUME WA DAR ALIYESUMBUA MIKOANI

  NA AYOUB HINJO     MARA nyingi wanaume wa Dar (Dar es Salaam) wamekuwa gumzo katika mitandao ya kijamii, ambako hutolewa mifano mingi ambayo uhalisia wake hufanana nayo kutokana na mazingira wanayoishi. Imezoeleka watu wanaoishi Dar es Salaam hupata wakati mgumu pindi wanapokuwa nje ya mkoa huo, kwasababu mahitaji yao mengi hupatikana kirahisi zaidi kuliko wanapokuwa mikoani. Pamoja na […]

NYOTA WANAOKIMBIZA LIGI YA KIKAPU DAR MSIMU HUU

NA SHARIFA MMASI   MAMBO yanazidi kupamba moto katika Ligi ya Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam, inayoshirikisha jumla ya timu 24, kati ya hizo 16 ni za wanaume na zilizobaki za wanawake. Tayari timu za wanawake zimeanza maandalizi kuelekea duru la pili la ligi hiyo, huku wanaume wakiendelea kumenyana kwenye mzunguko wa kwanza unaotarajiwa kufikia tamati wiki […]

MAVROPANOS NA MAKINDA HATARI ANAOWAACHA WENGER

LONDON, England   KIKOSI cha Arsenal kilichofungwa mabao 2-1 na Manchester United wikiendi iliyopita kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa katika dimba la Old Trafford, ni dalili nzuri za mwanzo mpya wa Arsenal bila Arsene Wenger. Mchezo ule ulikuwa ni jaribio zuri mno kwa vijana hao wadogo wa Arsenal waliopewa nafasi ya kuonesha uwezo wao dhidi ya mahasimu wakubwa […]

BURUDANI KIBAO EL CLASICO KING SOLOMON J’PILI

NA MWANDISHI WETU   WAPENZI wa soka nchini watakaofika kwenye ukumbi wa King Solomon, uliopo Namanga, Dar es Salaam kushuhudia pambano la Ligi ya Hispania ‘La Liga’ kati ya Barcelona na Real Madrid na Barcelona, watapata burudani kibao, ikiwamo nyama choma na vinywaji mbalimbali. Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa Azam Media, Tido Mhando, […]