Author: Bingwa

WASUGUA BENCHI SIMBA WATAJIJU

NA MWAMVITA MTANDA   KOCHA Mkuu wa Simba, Pierre Lechantre, amesema muda uliobaki kumaliza msimu ni mchache, hivyo hana muda tena wa kufanya kazi ya kuwahimiza wachezaji wanaoonekana kutojifahamu wanaosotea benchi. Awali, Piere alikuwa akitumia muda mwingi mazoezini kuwahimiza wachezaji wake wanaosotea bechi kufanya mazoezi kwa bidii ili waweze kupata nafasi ya kuwapo katika kikosi cha kwanza na hata kuingia […]

MSUVA WATAKA AJIB, YONDAN WAPOTEZEWE

  NA ZAINAB IDDY WINGA wa kimataifa wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa nchini Morocco, Simon Msuva, amewataka wachezaji wa timu yake ya zamani, Yanga, kuwapotezea nyota wa kikosi hicho waliokacha safari ya Algeria na badala yake kuipigania klabu yao hiyo na maisha yao kwa ujumla. Msuva anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya Difaa El-Jadida, juzi alipata nafasi ya […]

KANE ATAMANI KUIONGOZA ENGLAND

LONDON, ENGLAND STRAIKA wa timu ya Taifa ya England, Harry Kane, ameweka wazi kwamba, atakuwa na furaha kubwa endapo atapata nafasi ya kuwa nahodha wa timu hiyo kwenye fainali za Kombe la Dunia nchini Urusi. Kocha wa timu hiyo, Gareth Southgate, anatarajia kutangaza majembe yake Mei 15, ambayo atakwenda nayo nchini Urusi. Kocha huyo tangu amechukua nafasi ya kuisimamia timu […]

RODRIGUEZ AMKINGIA KIFUA ULREICH

MUNICH, Ujerumani | STAA James Rodriguez amemkingia kifua mwenzake, Sven Ulreich, akisema kuwa, hapaswi kulaumiwa kwa kosa alilofanya la kuwazawadia bao Real Madrid na kuwafanya watupwe nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Juzi Bayern iliweza kulazimisha sare ya mabao 2-2 ikiwa ugenini dhidi ya Real Madrid, lakini wakajikuta wakitolewa kwa jumla ya mabao 4-3. Katika mchezo huo, Ulreich […]

FELLAINI AMVAA CARRAGHER

LONDON, England KIUNGO wa Manchester United, Marouane Fellaini, amemvaa nyota wa zamani Liverpool, Jamie Carragher, akihoji alipotoa mamlaka ya kumkosoa wakati anakabiliwa na sakata la kumtemea mate mtu. Carragher alisimamishwa kuchambua soka katika televisheni, baada ya kunaswa na kamera akimtemea mtu ambaye walionekana kutofautiana lugha. Akizungumza juzi kuhusu maoni ambayo yaliwahi kutolewa na Carragher katika moja ya makala zake alizowahi […]

MOROCCO AKUBALI MIKOBA YA LWANDAMINA

NA TIMA SIKILO | KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’, Hemed Morocco, amesema yupo tayari kuinoa timu yoyote ikiwamo Yanga iliyotajwa kumpigia hesabu kubeba mikoba ya George Lwandamina aliyerejea katika kikosi chake cha Zesco ya nchini kwao, Zambia. Yanga kwa sasa wananolewa na Mzambia Noel Mwandila akisaidiana na Shadrack Nsajigwa, ikiwa ni baada ya kuondoka kwa […]

YANGA WAIFUATA USM ULGER NA HASIRA KIBAO

SAADA SALIM NA HUSSEIN OMAR | WAWAKILISHI pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa, Yanga, wameondoka Dar es Salaam jana kuelekea mjini Algiers, kuvaana na USM Alger ya Algeria katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika. Yanga ambayo itakuwa ugenini dhidi ya Waarabu hao, watashuka dimbani Jumapili hii, huku wakiwa na usongo wa kufanya […]

SIMBA HAINA HURUMA, WAITANGAZIA VITA NDANDA

CLARA ALPHONCE NA MWAMVITA MTANDA PAMOJA na kubakiza pointi tano tu kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba imepanga kutokuwa na huruma na timu yoyote watakayokutana nayo, ikiwamo Ndanda FC watakayoikaribisha Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam keshokutwa. Iwapo watashinda mchezo huo, Simba watabakiza pointi mbili tu kujitangaza mabingwa wapya wa ligi hiyo, taji walilolisotea kwa misimu mitano bila […]