Author: Bingwa

Mo awapa masharti vigogo Simba

*Awataka kufanya kila wawezalo Al Ahly, AS Vita wapigwe U/Taifa NA MWANDISHI WETU MWEKEZAJI wa Simba, Mohammed Dewji `Mo Dewji`, amecharuka na kuwapa masharti viongozi wa Bodi ya klabu hiyo, kusuka mikakati kabambe kuhakikisha wanawafunga Al Ahly ya Misri na AS Vita ya DR Congo katika michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika, katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mchezo […]

Simai: Tamasha la Sauti za Busara ni kichocheo cha uchumi wa nchi

Festo Polea, Zanzibar Mwenyekiti wa Bodi ya Busara Promotions, Simai Mohammed, amesema tamasha la Kimataifa la Muziki la Sauti za Busara ni kichocheo cha uchumi wa Zanzibar kupitia utalii kwa ujumla. “Kuanzia leo tutashudia burudani ya muziki kutoka kwa wasanii mbalimbali wa ndani na nje, wanamuziki hao wataonyesha nyimbo za tamaduni za nchi zao zenye mafunzo, burudani na jumbe mbalimbali […]

AMINI HIVYO…Kwa haya mawili, Emery hana kosa Emirates

LONDON, England KUNA presha fulani imeanza kumvaa kocha mwenye miezi nane tu kwenye kikosi cha Arsenal, Unai Emery. Wapo baadhi ya mashabiki wanaotaka atimuliwe. Emery aliuanza vizuri msimu huu, akicheza mechi takribani 22 bila kufungwa, lakini ghafla upepo ulibadilika mara tu walipotandikwa  na Southampton. Mwishoni mwa wiki iliyopita, waliporomoka hadi nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu baada ya […]

Guardiola: Ubingwa bado hauna mwenyewe

MANCHESTER, England KOCHA wa timu ya Manchester City, Pep Guardiola, amedai kuwa lengo lao la kutetea ubingwa wa Ligi Kuu England litakabiliwa na upinzani mkali hata kutoka kwa Manchester United na Chelsea. Man City ilitarajiwa kuchuana na Everton usiku wa kuamkia leo, huku wakiwa na lengo la kuwafikia kwa pointi vinara wa Ligi Kuu, Liverpool. Vijana wa kocha Jurgen Klopp, […]

WANASUKUMIA NYAVUNI

Vita ya mabao Ligi za Ulaya imenoga balaa LONDON, England MSIMU wa soka barani Ulaya umeingia katika kipindi cha lala salama, huku wapachika mabao wakizidi kuvutana mashati katika vita ya kuwania kiatu cha dhahabu kwa mfungaji bora wa 2018/19. Mshindi wa msimu uliopita, Lionel Messi, anatazamia kutetea taji lake baada ya kufunga mabao 34 kwenye La Liga ambayo yalimpa kiatu […]

Dimpoz atoa siri ya Bella kunogesha Ni Wewe

NA CHRISTOPHER MSEKENA STAA wa Bongo Fleva, Omari Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, amesema alimwomba Christian Bella aingize sauti yake katika wimbo mpya Ni Wewe ili kuunogesha zaidi. Dimpoz alisema Bella alimtembelea wakati anaumwa na alipomshirikisha wazo la Ni Wewe alilipenda na akajikuta ana ‘free style’ zile sauti zinazosikika mwishoni mwa wimbo huo. “Nikamwomba anisaidie kuingiza sauti yake kwenye wimbo wangu kwa […]

Johari afunguka kuwapa nafasi chipukizi

NA JEREMIA ERNEST MWIGIZAJI mkongwe nchini, Blandina Chagula ‘Johari’, amesema alilazimika kupumzika kwa muda ili kuwapa nafasi wasanii chipukizi kuonyesha uwezo wao na mwaka huu amejipanga kurejea tena kwa kishindo. Akizungumza na Papaso la Burudani, Johari, ambaye ni miongoni mwa wamiliki wa kampuni ya RJ inayozalisha filamu nchini, alisema kimya chake kilifanya wasanii wachanga kupata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao, […]

Coastal Union waapa ‘kufa na mtu’ Mkwakwani

NA MWANDISHI WETU, TANGA UONGOZI wa klabu ya Coastal Union, umeapa kuichapa timu yoyote ikayokutana nayo katika mchezo wa   Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini hapa. Akizungumza na BINGWA jana, Ofisa Habari wa Coastal Union, Hafidh Kido, alisema malengo yao ni kupata ushindi katika kila mchezo utakaopigwa kwenye uwanja huo. Kido alisema wakati wa kuwa wanyonge […]

Katwila: Hatukubali Lyon watufunge

NA SALMA MPELI WAKATI wakijiandaa na mchezo wao dhidi ya African Lyon kesho, kocha mkuu wa timu ya Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila, amesema wanahitaji kurejesha heshima yao kwa kuibuka na ushindi. Akizungumza na BINGWA jana, Katwila alisema wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanashinda ili wasogee katika nafasi za juu zaidi kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Mtibwa watashuka dimbani kuivaa Lyon […]

Zahera abaini mbinu za kuwafunga Simba

NA MWAMVITA MTANDA LICHA ya kikosi cha Simba kuwa na wachezaji bora wenye viwango vya kimataifa, lakini Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amebaini mapungufu yao yapo kwenye safu ya ulinzi. Zahera amegundua hili wakati akijiandaa kuvaana na mahasimu wao hao katika mchezo wa mzunguko wa pili ya Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaopigwa Februari 16, mwaka huu kwenye Uwanja wa […]