Author: Bingwa

DJUMA AWAPA YANGA UJANJA KIMATAIFA

CLARA ALPHONCE NA WINIFRIDA MTOI   *Atoa siri za kuimaliza Rayon *USM Alger yaitumia salamu   LICHA ya kuwatembezea kipigo cha bao 1-0 mahasimu wao Yanga, Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma, amesema timu hiyo ya Jangwani ina nafasi kubwa ya kufanya vizuri katika mechi za kimataifa endapo wataongeza juhudi za maandalizi. Simba iliwafunga Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu […]

SIMBA SC YAIZIDI KETE CAMEROON KWA PIERRE

NA SAADA SALIM   BAADA ya Simba kuibanjua Yanga bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita, wameamua kuifanyia kauzibe timu ya Taifa ya Cameroon ambayo inaweza kumnasa kocha wao, Pierre Lechantre. Mawakala wa Pierre, ambaye aliingia mkataba wa miezi sita na Simba, wametuma maombi nchini Cameroon kwa ajili ya kuomba kibarua hicho cha […]

WASHINDI MZUKA WA SOKA NA COCACOLA WAZAWADIWA

NA GLORY MLAY   WAKAZI 32 wa mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Singida, wamejishindia zawadi  mbalimbali ikiwamo pikipiki, runinga bapa za kisasa na fedha taslimu shilingi 100,000 kwenye promosheni ya Mzuka wa Soka na Cocacola. Akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi, Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Bonite Bottlers, Chris Loiruck, alisema kumekuwa na ongezeko la washindi katika wiki ya […]

ZIDANE ‘AWAJAZA SUMU’ NYOTA MADRID

MADRID, Hispania   KOCHA wa Real Madrid, Zinedine Zidane, ametaja wazi neno la mwisho alilowapa wachezaji wake kwamba, wanatakiwa kuhakikisha wanaonesha kiwango cha hali ya juu watakapoivaa Bayern Munich kesho kwenye mechi ya kesho ya nusu fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya. Zidane alisema hayo mara baada ya kikosi chake hicho kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Leganes kwenye […]

MOURINHO AMUAGA WENGER KWA KICHAPO, MANCHESTER UNITED IKIICHAPA ARSENAL 2-1

MANCHESTER, England   KOCHA wa Man United, Jose Mourinho, amempa mkono wa kwaheri mwenzake wa washika mitutu wa London, Arsenal, babu Arsene Wenger kwa kumtandika mabaon 2-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa jana katika dimba la Old Trafford. Mchezo huo ulikuwa ni wa mwisho kwa Wenger kuiongoza timu yake ya Arsenal kwenye dimba hilo la Old Trafford, baada […]

DAH! WAKIMALIZA URUSI, HUENDA NDIO BASI TENA KOMBE LA DUNIA

MOSCOW, Urusi   BADO miezi michache fainali za Kombe la Dunia zianze kutimua vumbi nchini Urusi, huku kila timu ikijipanga kufanya vyema katika michuano hiyo. Pamoja na fainali hizo kuanza Juni 14, kuna baadhi ya wachezaji wanaweza wasipate nafasi nyingine ya kucheza michuano hii mikubwa duniani, iwe kwa kustaafu au kuachwa kutokana na umri wao kuwa mkubwa. Makala haya yanakuletea […]

MASENTAHAFU WALIOTIKISA TANZANIA (3)

NA HENRY PAUL   WIKI iliyopita BINGWA lilikuletea baadhi ya wachezaji mahiri waliokuwa wanacheza safu ya kati ‘Masentahafu’, ambao walikuwa na uwezo wa kipekee na kutamba katika timu zilizokuwa zinashiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (sasa Ligi Kuu) na hata wengine kuchezea timu ya Taifa Stars. Wafuatao ni mwendelezo wa wachezaji hao ambao walivuma katika ligi zetu na hata […]

HASTA LA VISTA ANDRES INIESTA…

  TULIOBAHATIKA kuwa mashuhuda wa ustadi wake, Andres Iniesta, hebu tumuage kwa kusema, Hasta la Vista, kwaheri fundi. Kama shida ingekuwa inagonga hodi, halafu mtu mmoja kati yetu angekuwa na roho ngumu ya kuikaribisha, angekuwa msaada mkubwa kwa Iniesta. Kabla ya kuifafanua hiyo kauli, ngoja kwanza nipooze koo kwa maji yasiyo na ubaridi. Nahisi ninapoandika maneno haya ni kama vile […]

SIMBA WAIPIGA YANGA

NA WAANDISHI WETU   VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba, wamewachapa mahasimu wao Yanga bao 1-0 na kubakiza pointi tano kuweza kunyakua ubingwa wao wa kwanza tangu mwaka 2012. Mchezo huo wa marudiano uliopigwa jana kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu kubwa kwani ndio ambao ungeweza kutoa taswira ya Simba kuwa mabingwa au […]