Author: Bingwa

Mzee wa Bwax atoa siri ya kuitwa ‘Mtoto wa nje ya ndoa’

KARIBU msomaji wa Jiachie na Staa Wako, safu inayokupa nafasi ya kusoma majibu ya mastaa mbalimbali katika tasnia ya burudani kupitia maswali waliyoulizwa na mashabiki. Leo hii tupo na Mohammed Said ‘Mzee wa Bwax’ miongoni mwa nyota wa muziki wa singeli Bongo, anayetamba na ngoma kama Kisimu Changu, Unaringa Nini, Kisulisuli na nyinginezo. SWALI: Juma Paul kutoka Kigoma anauliza: “Ulianza […]

Unatamani uishi katika mahusiano ya namna ipi? Fanya hivi upate unachotaka

AMANI na furaha ni sababu ya kwanza ya watu kuingia katika mahusiano. Lakini jiulize, umejiandaa kuitengeneza? Kama ilivyo kwa vitu vingine, furaha katika mahusiano pia ina misingi yake. Unaijua na uko tayari kuifuata? Wengi ukiwauliza hilo swali wataitikia ila hawatojitolea kwa vitendo na kauli kwa ajili ya misingi ya furaha katika mahusiano yao. Moja ya kanuni muhimu ya kupata furaha […]

The Mafik: Hakuna kama Mbalamwezi

NA JEREMIA ERNEST MIEZI mitatu baada ya kifo cha mwanamuziki wa The Mafik, Mbalamwezi, kundi hilo limesema halina mpango wa kuongeza msanii mwingine sababu hakuna mtu mwenye uwezo wa kuziba pengo hilo. Akizungumza na Papaso la Burudani hivi karibuni miongoni mwa wasanii wanaounda kundi hili, Hamadai alisema hawana mpango wa kuongeza msanii mwingine zaidi ya kuendeleza mipango waliyopanga na Mbalamwezi. […]

Mastaa waguswa na mkasa za mtoto Anna

NA MWANDISHI WETU TUKIO la mwanafunzi aliyefichwa taarifa za vifo vya wazazi wake na wadogo zake watatu, Anna Zambi, limewagusa watu mbalimbali nchini wakiwamo mastaa wakubwa kwenye tasnia ya burudani. Anna Zambi (16) ambaye alikuwa anasoma kidato cha nne katika shule ya Mather Theresia of Calcuta mkoani Kilimanjaro, alipewa taarifa hizo za kusikitisha mwishoni mwa wiki ikiwa ni siku 22 […]

Diamond, Harmonize jukwaa moja Dubai

CHRISTOPHER MSEKENA TAMASHA kubwa la muziki Dubai, One Africa Music Festival, linatarajiwa kufanyika usiku wa leo katika ukumbi wa matamasha (Festival Arena) na kuwakutanisha wasanii, Diamond Platnumz na Harmonize. Mapema mwezi uliopita Harmonize alitangaza kuacha kufanya kazi na WCB inayomilikiwa na Diamond Platnumz na kutambulisha uongozi wake wa Konde Music Worldwide hivyo kufanyika kwa tamasha hilo Dubai, kutaweza kuwakutanisha. Mbali […]

Mkongwe Arsenal awaambia mashabiki wampe muda Pepe

LONDON, England  MKONGWE wa Arsenal, Thierry Henry, amewataka mashabiki wa timu hiyo kumpa muda winga wao bei ghali, Nicolas Pepe, kuzoea mazingira ya Ligi Kuu England. Pepe bado hajaonyesha kiwango chake bora, alichokuwa nacho wakati anakipiga Lille ya Ufaransa msimu uliyopita. Hata hivyo Henry anaamini Pepe ataonyesha makali yake endapo mashabiki watamvumilia. “Watu wanatakiwa kuelewa, kujiunga na klabu kubwa kama […]

Hudson-Odoi amtaja aliyembakisha Chelsea

LONDON, England  WINGA wa Chelsea, Callum Hudson-Odoi, amesema ilichukua mazungumzo ya muda mchache cha bosi mpya, Frank Lampard, kumshawishi ambaki Stamford Bridge. Nyota huyo wa miaka 19 aliwasilisha maombi ya kuondoka baada ya Chelsea kukataa ofa ya pauni milioni 35 kutoka kwa Bayern Munich. Hata hivyo mwishoni mwa msimu uliopita, alifanikiwa kupenya kwenye kikosi cha Maurizio Sarri na amemfurahisha Lampard […]

Hili la Mkude kama sinema

NA MWANDISHI WETU HABARI ndiyo hiyo kuwa Jonas Mkude ni miongoni mwa wachezaji wenye thamani kubwa mno ndani ya Simba na hata timu ya Taifa, Taifa Stars, japo wengi wamekuwa wakimtafsiri tofauti, imebainika. Uchunguzi uliofanywa na BINGWA, umebaini kuwa kiungo huyo ametokea kuwateka makocha wa timu zote hizo mbili, kwa maana ya Patrick Aussems wa Simba na Etienne Ndayiragije wa […]

USAJILI YANGA KUFYEKA VIGOGO

MICHAEL MAURUS JAPO kwa sasa wanaonekana kuwa kimya, wapenzi wa Yanga kuna kitu wanasubiri kuona kama kinaweza kuwafuta machozi baada ya kuunza msimu huu kwa ‘kuungaunga’. Wakati wakijiandaa kuupokea msimu huu, wapenzi wa Yanga walikuwa na matumaini makubwa ya kufanya makubwa, hasa Ligi Kuu Tanzania Bara. Kati ya mambo yaliyokuwa yakiwapa jeuri hiyo, ni kocha wao Mwinyi Zahera aliyejijengea imani […]