Author: Bingwa

NDUDA KUVUNJA MKATABA SIMBA

NA GLORY MLAY MLINDA Mlango wa klabu ya Simba, Said Mohamed ‘Nduda’, amesema yuko tayari kuvunja mkataba na klabu hiyo endapo atatolewa kwa mkopo kwa timu nyingine. Akizungumza na BINGWA jana, Nduda alisema hayupo tayari kucheza klabu nyingine yoyote Tanzania Bara, hivyo anahitaji kuwa huru ili kuweza kutafuta maisha sehemu nyingine. “Nina mpango huo wa kuvunja mkataba na Simba, kwani […]

SIMBA YAZIDI KUNOGA

NA WINFRIDA MTOI *Yawanasa wababe wa USM Alger iliyoitoa nishai Yanga *Djuma atamba; Mkude, Kwasi watuma salamu MAMBO yamezidi kunoga katika kambi ya Simba nchini Uturuki baada ya timu ya Jeunesse Sportive de la Saoura maarufu JSS ya Algeria, kufuatilia mazoezi yao yanayoendelea huko. JSS ni moja ya timu kubwa nchini Algeria iliyoweza kuwafunga wababe wa Yanga, USM Alger mara […]

YANGA MAMBO NI MOTO

NA TIMA SIKILO *Mrithi wa Rostand huyu hapa, waliogoma waanza tizi kibabe *Matajiri tayari kumwaga fedha iwapo ‘kirusi’ kilichobaki Jangwani kitaondoka HATIMAYE mambo yameanza kunyooka Yanga baada ya wachezaji waliokuwa wamegoma kuripoti mazoezini jana, huku matajiri wakitangaza azma yao ya kumwaga fedha Jangwani lakini tu iwapo mmoja wa wajumbe wa kamati za klabu hiyo, ataondoka. Mjumbe huyo ni yule anayetajwa […]

KLOPP AMVULIA KOFIA PULISIC KWA KUWATUNGUA

NEW YORK, Marekani KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp, amemsifia staa anayemfukuzia, Christian Pulisic, baada ya kinara huyo wa Borussia Dortmund kuwatungua mara mbili na hivyo kumfanya akune kichwa zaidi jinsi atakavyopambana katika mechi za Kombe la Kimataifa. Katika mchezo huo ambao ulipigwa juzi katika Uwanja wa Bank of America United, nyota huyo alifunga mabao mawili ambayo yaliifanya Dortmund kutoka nyuma […]

MZEE JENGUA: MIMI NI MWEMA, SANAA IMEFANYA NIONEKANE KATILI

KARIBU msomaji wa Jiachie na Staa Wako, safu inayokukutanisha na watu  maarufu kutoka sekta mbalimbali ndani na nje ya Bongo, ili upate kufahamu mambo mengi kutoka kwao, karibu. Leo tupo na Mohammed Fungafunga maarufu kama Mzee Jengua, mkongwe wa sanaa ya uigizaji nchini akiwa amejizolea heshima kwa kuvaa uhusika wa mtu katili katika filamu zake ikiwamo tamthilia ya hivi karibuni […]

WARAKA WA OZIL KULALAMIKA KUBAGULIWA UJERUMANI -1

MUNICH, Ujerumani KIUNGO wa Ujerumani, Mesut Ozil, ametangaza kustaafu kuitumikia timu ya taifa kutokana na sababu za ubaguzi zinazoendelea juu yake. Ozil mwenye umri wa miaka 29, alibainisha hayo juzi baada ya kutumia akaunti zake za mitandao ya kijamii akibainisha hayo huku akimhusisha Rais wa Shirikisho la Soka Ujerumani (DFB), Reinhard Grindel, katika sakata hilo. Kiungo huyo aliyecheza michezo 92 […]

UJIO WA WAGENI NCHINI UWAFUNDISHE KITU WASANII WETU

NA CHRISTOPHER MSEKENA HAKUNA kinachoweza kupinga ukweli kuwa Tanzania ndiyo nchi namba moja kwa sasa katika sekta ya burudani ikifuatiwa na Kenya katika Ukanda huu wa Afrika Mashariki. Muziki wa Bongo Fleva umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuukimbiza ule wa Nigeria na Afrika Kusini kwenye ‘main stream’, kiasi cha mashabiki wa Afrika Mashariki kutumia zaidi nyimbo za Bongo Fleva katika matumizi […]

ZAYD ATUA BIDVEST WIST KWA MAJARIBIO

NA SAADA SALIM BAADA ya uongozi wa Azam FC kufanikiwa kumuuza Shaban Iddi `Chilunda`, nchini Hispania, milango imefunguka kwa kinda wake mwingine, Yahya Zayd, aliyeondoka nchini jana kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya majaribio katika klabu ya Bidvest Wist inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo. Zayd alikuwa mchezaji tegemeo ndani ya kikosi cha timu hiyo kwa msimu uliopita, baada ya kucheza […]